Magnificient
JF-Expert Member
- Aug 8, 2013
- 1,162
- 705
Salaam wana Jf, salaam sana. Nimekuwa nikijichanganya mazungumzo na wasomi wetu na kuangalia nyendo zao za sasa, nilichoambulia ni masikitiko tu. Hivi inakuaje mtu hadi anagraduate hajapata hata wazo moja la maisha? Fikra zote ni kupata cheti, na baada ya hapo ni kutafuta na kufanya kazi; iwe aliyosomea au la. Na hata huko kazini mawazo ni yale yale, hakuna ubunifu wala njia mpya! Yaani utamkuta kila siku anafanya yale yale kwa njia zile zile ilhali anajua shida zote na changamoto zake. Njoo kwa ambao hawajapata kazi sasa, utachoka! Hakuna analobuni wala kujaribu zaidi ya kufanya kazi za muda kujishikiza, nako ni kufanya yale yale. Yaani asipokuta kitu kimeanzishwa ndio basi tena, yeye haanzishi na wala hafikiri tofauti. Kwa kweli ni hasara, hushindwa hata kuwa msaada kwa wengine ambao hawajaenda shule au chuo. Rai yangu ni kila mhitimu ajitahidi kubuni vitu na njia mpya, na afikiri tofauti; vinginevyo tutabaki na maisha haya haya. Umasikini, rushwa, ukosefu wa ajira, gharama kubwa za maisha n.k. !