SoC04 Wahitimu wote wa vyuo wajitolee katika sekta ya umma mwaka mmoja

SoC04 Wahitimu wote wa vyuo wajitolee katika sekta ya umma mwaka mmoja

Tanzania Tuitakayo competition threads

luhanga7

New Member
Joined
Dec 19, 2013
Posts
4
Reaction score
2
Tanzania ni moja ya nchi ambayo inapiga hatua katika nyanja mbalimbali za maendeleo kama elimu, afya, madini, maji, utalii, kilimo, uvuvi nk.

Katika sekta zote hizo, sekta ya elimu imekuwa sekta mama kwasababu ndio imekuwa ikizalisha wataalamu wanaohudumu katika sekta zingine.

Mfumo wetu wa elimu umekuwa ukiboreshwa na serikali kadiri miaka inavyosonga mbele ili kuendana na mahitaji ya wakati husika.

Hivi karibuni tumeona serikali imeboresha mitaala ili iweze kutoa wataalamu wanaoendana na zama hizi ambazo zina ushindani mkubwa.

Kwa miaka kadhaa katika nchi yetu ya Tanzania tumeshuhudia uhaba wa watumishi katika katika sekta ya umma kama elimu, afya, maji nk. Hili limepelekea utolewaji wa huduma zilicho chini ya kiwango kwa wananchi.

Serikali imejitahidi sana kuboresha miundombino ya Shule, hospitali, maji, umeme, Barbara nk. lakini wafanyakazi wa serikali katika maeneo hayo wamekuwa hawatoshi.

Uchache huu wa wafanyakazi unatokana na ufinyu wa bajeti na uwezo serikali kuwa mdogo kwa wakati huo kuajiri wafanyakazi wengi.

Ili kuboresha na kuwa na wafanyakazi wengi serikalini napendekeza kwamba wahitimu wote wa vyuo wa fani tofauti tofauti wajitolee katika sekta ya umma kwa mwaka mmoja mmoja. Kitendo hili kiwe lazima kama inavyokuwa kwa wanafunzi wanaomaliza kidato cha sita kwenda JKT kabla ya kuingia elimu ya juu. Wahitimu hao wanaweza jitolea katika maeneo ambayo wanatokea ili kupunguza gharama za maisha wakiwa wanajitolea au sehemu yoyote ile ya Tanzania.

Faida za wahitimu kujitolea ni kama ifuatavyo:
(i) Wahitimu watapunguza uhaba wa watumishi serikalini
-kwa mwaka mzima wahitimu hawa watafanya kazi hivyo ombwe la upungufu wa wafanyakazi litapungua bila gharama.

(ii) Wahitimu wanapata uzoefu wa kazi
-Siku hizi kuna changamoto kubwa sana ya waajiri kusema kwamba wahitimu wengi hawana uzoefu wa kazi pindi tu watokapo chuoni. Kupitia wazo hili tatizo hilo litapungua kwa kiasi kikubwa.

(iii) Mchakato huu utakuza uzalendo kwa wahitimu
-kufanya kazi kwenye ofisi za umma kwa mwaka mzima kwa kujitolea kwa moyo kwa wahitimu hawa itaongeza uzalendo wa kuipenda na kuithamini nchi yetu.

(iv) Mchakato huu utatoa muda kwa serikali kujipanga kuongeza wafanyakazi
-serikali mara zote uajiri wafanyakazi pale inapokuwa na na uwezo wa kibajeti, hivyo wahitimu wanavyojitolea serikali inapata muda wa kujipanga na kuajiri zaidi wafanyakazi bila presha huku wananchi wakipata huduma bora.

(v) Mchakato huu utapunguza gharama za serikali katika uendeshaji wake
-Wahitimu Hawa watakuwa wanajitolea hivyo hawatokuwa wanalipwa kama wafanyakazi wengine walioajiriwa, hivyo gharama za mishahara zitapungua na pesa hizo zitapelekwa katika maeneo mengine.

Namna ya kufanya Mchakato huu ni kwamba baada ya wanavyuo kumaliza masomo yao serikali itawapangia maeneo yao ya kujitolea wote ambayo watakuwa katika ofisi au sehemu hizo wakifanya kazi ya kujitolea kwa mwaka mmoja.

Baada ya kupangiwa maeneo yao wahitimu hao wataripoti na kufanya kazi huku wakisimamiwa na kupewa vigezo vya ufanisi na siyo bora liende tu. Serikali itaandaa muongozo wa kufanya Mchakato huu kwa tija.

Baada ya kumaliza mwaka mmoja wa kujitolea, wahitimu hao watapewa vyeti ambavyo watavitumia kuombea ajira za kudumu serikalini au sekta binafsi. Kuwekwe utaratibu kwamba muhitimu asiajiriwe sekta ya umma au binafsi bila hicho cheti cha kujitolea kwa mwaka mmoja. Cheti hicho kinaweza kutolewa na mamlaka yoyote ya serikali ambayo itapewa jukumu hilo kwa umakini na uaminifu mkubwa.

Mwaka mmoja ukiisha kundi moja linamaliza na lingine linaingia, yaani mchakato unakuwa endelevu mpaka pale serikali itakapokuwa na watumishi wa kutosheleza.

Tanzania tuitakayo yenye watumishi wa kutosha wa kutoa huduma bora kwa jamii inawezekana kwa mchakato huu wa wahitimu wote wa vyuo kujitolea katika sekta ya umma.
 
Upvote 4
Asante sana, naamini kupitia Jamii forum Stories of Change itawafikia wengi ikiwemo mamlaka zenye kufanya maamuzi ya nchi.
 
Back
Top Bottom