Wahubiri mabalozi wa Serikali ya Zimbabwe walivyokamata soko la wahubiri vijana wa injili Tanzania

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Anaandika Habibu B. Anga,

Sadaka ni sehemu ndogo ya source ya utajiri wao.
Kizazi kipya cha wachungaji vijana wana formula mpya kali mno.
Tony Kapola (Ubert Angel) -Zimbabwe
Clear Malisa (Passion Java) - Zimbabwe
Huyu pichani David Richard (Edd Branson) - Zimbabwe
Siku moja tujadili what is happening.

Kwa mfano; Moja ya Prophet machachari kijana kwa sasa ni Clear Malisa wa kanisa la ‘Kingdom Embassy’ Ubungo Riverside. Malisa anafanyakazi chini ya Passion Java toka Zimbabwe.
FYI: Huyu Passion Java pia ndiye aliyelipa fidia ya bilioni 1.6 ili Rayvanny avunje mkataba Wasafi…

Mfano #2: Mchungaji pendwa Tony Kapola anafanya shughuli zake chini ya Mentorship ya Ubert Angel pia wa Zimbabwe.
Ubert Angel pia ni ‘kijana’ wa Rais Mnangagwa, tena kijana wa anayeaminiwa haswa kiasi kwamba mpaka Mnangagwa akampa hadhi maalumu ya Ubalozi (Ambassador At Large)..

Mfano #3: Mdogo wetu DALE wa Angels Ministries, Mbezi Beach Tangi Bovu, yuko chini ya Edd Branson naye toka Zimbabwe.
Edd Brason pia ni ‘kijana’ anayetegemewa mno na Rais Mnangagwa kiasi kwamba amepewa pia hadhi ya Ubalozi (Balozi mwenye ‘kazi maalumu’)
Sijui mmeanza kuelewa??
 
Nimeishia hapo kwenye Bilioni 1.6 atakayemalizia atasimulia
 
kwa msiojua, chuo kikuu cha uchawi kwenye ulimwengu wa giza huko, kipo zimbabwe. wachawi halisi watawaambia hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…