Wahubiri wakristo acheni kudhalilisha jina la Yesu

Wahubiri wakristo acheni kudhalilisha jina la Yesu

raslimali

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2014
Posts
1,958
Reaction score
1,744
Biblia inasema muonye mtu muovu, la sivyo damu yake nitaitaka mikononi mwako. Ninyi wahubiri, manabii na mitume wa kisasa mnajua kweli nguvu ya jina la Yesu? Hi
li siyo jina la kutamka hovyohovyo. Unakemea sijui pepo sijui laana nusu saa nzima unataja jina la Yesu. Kwa jina la Yesu, kwa jina la Yesu................! Mmetoa wapi huu upumbavu? Tuna mfano wa namna hii kwenye maandiko? Huyo Yesu wenu ni mwingine. Mmefanana na wale manabii wa Baali kabisa waliopiga kelele siku nzima kumtaja Baali. Jina la Yesu wa kweli linatajwa mara moja na linakamilisha ombi. Tunadhalilisha imani ya kikristo. Acheni hayo mazingaombwe yenu. Huo siyo ukristo na mwisho Yesu atawaambia wazi SIWAJUI. Huko maredioni mnalidhslilisha jina la Yesu mchana na usiku. Huyo Mungi wenu kiziwi. Kwa wasio wakristo naomba muelewe huo siyo ukristo. Hao wana Mungu wao mwingine japo wanatumia biblia. Na miujiza shetani pia anayo!
 
Nipo hapa kuna redio moja mhubiri zaidi ya mara hamsini sasa KWA JINA LA YESU, KWA DAMU YA YESU.....!! Anakemea laana kwenye mkutano!
 
Wanadhailisha jina la Yesu. Ipo siku moto utashuka uwale. Kazi yao kupigana mieleka na mapepo na laana usiku kucha as if Yesu hakufanya kazi yoyote. Watakiona cha mtema kuni. Na ninyi mnaofuata miujiza huko dawa yenu iko jikoni na mtanyweshwa maana mmekuwa wapumbavu. Hamtaki kuweka mahusiano mazuri na Mungu ili muwe watoto wake na mpate kupewa naye mahitaji yenu sasa mmebaki kutafuta kuombewa na kuuziwa visaidizi kama maji na mafuta. Ole wenu!
 
Nawaomba watu wa imani zingine kama ndugu zetu waislamu ambao huwa wanasikiliza haya mambo redioni na kwenye mitandao wajue kwamba upuuzi huu si sehemu ya imani halisi ya Ukristo. Ukristo halisi una kanuni zake. No wonder even among more than 2000 sects there is no theological harmony within them! Hata Yesu alisema ufalme uliogawanyika hauwezi kudumu. Wanachafua imani halisi kwa tamaa zao binafsi. Their end is near.
 
Narudi tena kuwaonya wakristo waachane na huu upuuzi wa mitume na manabii feki. The church had since its inception a well formed structure ndiyo maana paliwekwa kanuni ya KUWEKEWA MIKONO ( Laying of hands) . Siyo kila mtu tu aamke asubuhi ajitangaze yeye ni mtume au nabii. Huu ni upumbavu na uzushi na ninarudia tena watu wa imani zingine wapuuzeni watu hawa maana si wakristo halisi. The real christianity is built on the foundation of apostles.
 
Ila kuna baadhi ya watumishi wamevamia fani Mara baada ya life kuwa piga kitaa
 
Hizi imani za mashariki ya kati zinatugawa sana .
 
Back
Top Bottom