Wahubiri wakristo, mitume, manabii walimu na kadhalika neno madhabahu msilitumie kutapeli watu

Wahubiri wakristo, mitume, manabii walimu na kadhalika neno madhabahu msilitumie kutapeli watu

raslimali

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2014
Posts
1,958
Reaction score
1,744
Madhabahu ilikuwa ni mahali pa kutolea sada za damu katika agano la kale. Siku hizi wahubiri wakristo wakianzisha kanisa wanaita madhabahu eti watu walete pesa hapo. Huu ni wizi na watu wengi wajinga wasioijua hata hiyo biblia ndio wamejazana huko. Utapeli mtupu.
 
Nataka tu niseme hayo ni zaidi ya mauaji ya halaiki. Watu wanalishwa mafundisho ya upumbavu. Ina maana mtu akianzisha utapeli kwa jina la Yesu mamlaka za nchi haiwezi kumshushulikia??? Tunaachia taifa letu liangamie hivi? Mbona matapeli wengine wanashughulikiwa vizuri? Mtu akisema utapeli kwa jina la Yesu basi anaachwa anapeta kwa raha zake akiwanywesha watanzania mihadarati ya kiimani na kuendelea kulirudisha taifa letu nyuma. Why????
 
Akili tuliyoumbwa nayo tuituime vizuri for the bettement of our lives. Nilishawauliza humu hawa wahubiri wa miujiza ya kuponya watu kwa nimi hawajawahi kumponya amputee ( aliyekatwa mguu au mkono) wote walikimbia hakuna aliyejibu. Mahubiri yao na uhalisia ni vitu viwili tofauti. Miujiza miujiza miujiza. Mbona hio hamuufanyi? Huyo Yesu wenu mwingine kabisa
Hawezi hilo!
 
Viwete wamejaa huko barabarani hakuna hata mmoja aliponywa kwenye hiyo mikutano yenu. Mnaliharibu taifa na kuligeuza taifa la wapumbavu na mataahira kwa uchu wenu wa utajiri. Huo ni utapeli na iko siku Mungu atasema enough is enough. Mmewapotosha maelfu ya watu na kuwaibia pesa zao kwa ulghai wa aya za biblia. Ole wenu!
 
Nilishasema wenye mamlaka tuliyowakabidhi kwa kura zetu liangalieni tatizo hili ili mwisho wa maisha msipite mbele ya kiti cha hukumu kujibu kwa nini mliachia mambo haya. Kutaja jina la Yesu sasa watu matapeli wanajificha kwenye hicho kichaka kwa amani wakijua mkono wa dola hautawagusa. Wanaharibu taifa letu kwa mafundisho potofu yenye kulemaza akili za za watu. Wala hayo siyo mafundisho ya kikristo ni utapeli tu wa kutengeneza pesa. Mamlaka japo zinasema hazina dini naomba ziangalie hili. Siyo mpaka watu wafe kimwili ndipo mchukue hatua. Watu wanauawa kiakili kila siku.
 
Ni vitu viwili tofauti. Wahubiri wa mjini ni wezi.
Wametengeneza madhabahu zao kwa ajili ya kukusanya hela.

Asante. Hapo unaona ufafanuzi huo na maana inayohubiriwa na wahubiri wa mjini inafanana auu??? Ni vitu viwili tofauti!
 
Back
Top Bottom