KERO Wahudumu kituo cha Mwendokasi Kibamba hawana huduma nzuri kwa wateja

KERO Wahudumu kituo cha Mwendokasi Kibamba hawana huduma nzuri kwa wateja

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Habari,

Kituo cha Kibamba wahudumu pale ni kero kubwa wana majibu ovyo, imeshakuwa kero kubwa itafikia hatua wananchi watajichukulia sheria mkononi.

Pia Dada anayekatisha tiketi ukidai Tsh 50 chenji anasema hana na ndio kinara wa kutoa majibu.

Tunaomba uongozi wa DART Mwendokasi mfanyie kazi hilo suala ikiwezekana chukueni maoni ya wadau pale ndo mtajua ukweli wa uovu waoo
 
Ngoja waarabu wata install automated system.
 
Kwani wahudumu wa mwendokasi wa wapi wana huduma nzuri?
 
Habari,

Kituo cha Kibamba wahudumu pale ni kero kubwa wana majibu ovyo, imeshakuwa kero kubwa itafikia hatua wananchi watajichukulia sheria mkononi.

Pia Dada anayekatisha tiketi ukidai Tsh 50 chenji anasema hana na ndio kinara wa kutoa majibu.

Tunaomba uongozi wa DART mfanyie kazi hilo suala ikiwezekana chukueni maoni ya wadau pale ndo mtajua ukweli wa uovu waoo
Duh sasa wewe unataka majibu mazuri kwa huduma ipi labda, mimi nawashangaa sana watanzania, limradi limeshajifia nyie mnahangaikaaaaaaaaa simtafute usafiri mwingine? kwani ni lazima hao jamaa , kwanza mabasi hawana sasa unahangaika na tiketi ili upande nini? watanzania aliyewaroga kawapatia sana.
 
Wananchi na ninyi mmezidi upole sana.yaani Hela Yako halafu huyo mwajiriwa akuambie chenji Hana na lugha za hovyo na wewe umenyamaza tu!Mimi skubali huo upuuzi.
 
Enzi hz za CHURA sahau kuhusu huduma nzuri!!!






KAZI ni kipimo cha UTU
 
Sh 50 abiria wanazoacha zinaenda wapi? Maana kama ni Udart wao wanahesabu pesa iliyoandikwa kwenye tiketi. Kuanzia asubuhi hadi jioni mamia ya abiria wanaacha sh 50 kwa kuambiwa hakuna chenji, je nani qnqchukua pesa hizo ambazo ukijumlisha kwa siku ni pesa nyingi sana.
 
Sio hao tu, UWAJIBIKAJI ni tatizo kubwa kwetu tanzania, haswa haswa haya maofisi ya serikali ndio kumeoza zaidi, mtu akiwa pale anajiona zaidi ya keki, maringo na mapozi kibao, atakuchangamkia kutokana na muonekano wako, yaani ni wachache saana wenye uwajibikaji na utu juu yake.
 
Back
Top Bottom