Bado Hujasema
Member
- Dec 1, 2024
- 12
- 14
Pale Kivukoni sehemu ya kukatia tiketi katika Kituo cha Mwendokasi pa hovyo sana.
Kwanza abiria ni wengi wanasongamana mno wanagombea tiketi. Mtu unakomaa kwenye foleni hadi unafanikiwa kufika dirishani, hapo unakuwa umepambana hasa.
Sasa unafika dirishani unataka ukate tiketi fasta fasta uwahi usafiri unakutana na mhudumu ambaye furaha yake ni kukuharibia siku.
Leo nimekutana na mkaka amekaa dirisha la kushoto, kijana jeuri sana yule na anaonesha hana adabu wala hajali kuhusu sisi wateja, anahudumia Watu kama tunasafiri bure au anatupa msaada. Anatoa majibu ya jeuri wala hajali kumkosea mtu heshima mbele ya wengine.
Anasema hana chenji, nikamuuliza kwahiyo nifanyeje? Akajibu "Kaa pembeni kama unaona nakuchelewesha, kapange foleni nyingine"
Acheni kufanyia watu wazima dharau tena mnawajibu kama mnaongea na wahuni kijiweni.
Hii sio mara ya kwanza kutokea changamoto ya chenji, kila mara nimeshuhudia hali hiyo ambayo imekuwa chanzo cha ugomvi na kupishana kauli baina ya Abiria na Wakatishaji tiketi.
Kwani hao wahusika hawawezi kutafuta njia mbadala badala ya kumpa kazi Abiria awe anatafuta chenji mwenyewe? Hawaoni kama suala hilo ni kero kubwa?