Wahuni hawakuwahi kuwa watu wazuri hata siku moja, kwenye shoo ya akina Juma Nature walikinukisha

MtotoKautaka

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2018
Posts
373
Reaction score
895
Wakuu Achimwene!!!!

Kuna siku nilienda kuhudhuria tamasha la wasanii walikuja hapa mkoani kwetu wakitokea Dar.

Wasanii waliokuja asilimia 80 walikuwa ni ma legend mf..nature, Daz baba, Linna, Fido vato, n.k.

Sasa kitu kilichonishangaza kuhusu wahuni wa hapa ni ukorofi na ubishi wao.

Jamaa walikuwa washajipigilia mibangi na mipombe, walikuwa na mi vibe ya hatari.

Ikafika zamu ya juma nature, ikaingia na wimbo wake wa hakuna kulala hata kama hujala. Jamaa wakawaka zaidi, huku wale migambo walinda amani na utulivu wakawa wanawatuliza wasipande juu jukwaani.

Jamaa wakawa hawaelewi, ikabidi migambo waanze kutumia virungu.

Eeeeeeh!!!! Na hilo ndilo kosa walilolifanya ambalo wanalijutia pengine mpka muda huu.

Wale wahuni walimvizia mambo mmoja wakamkamata mguu mmoja wakaanza kumvutia chini, wale migambo walokuepo juu wakamshika mwenzao mikono wakaanza kumvutia juu ili kumnusuru.

Wahuni wakaonekana kuwashinda migambo nguvu ikabidi migambo waongezeke juu, wakaongezeka migambo kama 3 hivi lakini bado wakawashinda nguvu.

Mwisho wa picha mgambo akafikishwa chini.

Wakuu kama kuna rangi ambayo hakuiona yule mgambo siku ile basi sijui ni ipi labda bado haijagunduliwa.

Yule mgambo alipigwa akavuliwa mabuti yake akapokonywa na kirungu chake.
Kiukweli binafsi nilimuonea huruma sana sana sana.

Hamuwezi amini na mpka sasa namimi bado sijaelewa kwanini ilikuwa vile, trust me wale wahuni walimuachia yule mgambo baada ya mimi kwenda na kuanza kuwa-please wamuachie.

Imagine wahuni wamewaka wanampiga sana lakini nikajitosa nikaenda kumtetea msela katikati ya vurugu na siyo kwamba mm ni mbavu kuliko wao hapana nilienda na maneno yangu tu wahuni wakamuachia mwamba akanishukuru kwa kunipa tano then akasepa.

Yule mgambo sikumuona tena nahisi alienda kulala kabisa.

All In All Muhuni ni mtu wa ajabu sana.
 
Attachments

  • IMG_20241107_230637.jpg
    IMG_20241107_230637.jpg
    265 KB · Views: 4
  • IMG_20241107_232043.jpg
    IMG_20241107_232043.jpg
    393.4 KB · Views: 5
Maana yake Mgambo wanaruka na kukanyagana
kibaya zaidi wote wameinama na wanaruka kinyama.
 
Wakuu Achimwene!!!!

Kuna siku nilienda kuhudhuria tamasha la wasanii walikuja hapa mkoani kwetu wakitokea Dar.

Wasanii waliokuja asilimia 80 walikuwa ni ma legend mf..nature, Daz baba, Linna, Fido vato, n.k.

Sasa kitu kilichonishangaza kuhusu wahuni wa hapa ni ukorofi na ubishi wao.

Jamaa walikuwa washajipigilia mibangi na mipombe, walikuwa na mi vibe ya hatari.

Ikafika zamu ya juma nature, ikaingia na wimbo wake wa hakuna kulala hata kama hujala. Jamaa wakawaka zaidi, huku wale migambo walinda amani na utulivu wakawa wanawatuliza wasipande juu jukwaani.

Jamaa wakawa hawaelewi, ikabidi migambo waanze kutumia virungu.

Eeeeeeh!!!! Na hilo ndilo kosa walilolifanya ambalo wanalijutia pengine mpka muda huu.

Wale wahuni walimvizia mambo mmoja wakamkamata mguu mmoja wakaanza kumvutia chini, wale migambo walokuepo juu wakamshika mwenzao mikono wakaanza kumvutia juu ili kumnusuru.

Wahuni wakaonekana kuwashinda migambo nguvu ikabidi migambo waongezeke juu, wakaongezeka migambo kama 3 hivi lakini bado wakawashinda nguvu.

Mwisho wa picha mgambo akafikishwa chini.

Wakuu kama kuna rangi ambayo hakuiona yule mgambo siku ile basi sijui ni ipi labda bado haijagunduliwa.

Yule mgambo alipigwa akavuliwa mabuti yake akapokonywa na kirungu chake.
Kiukweli binafsi nilimuonea huruma sana sana sana.

Hamuwezi amini na mpka sasa namimi bado sijaelewa kwanini ilikuwa vile, trust me wale wahuni walimuachia yule mgambo baada ya mimi kwenda na kuanza kuwa-please wamuachie.

Imagine wahuni wamewaka wanampiga sana lakini nikajitosa nikaenda kumtetea msela katikati ya vurugu na siyo kwamba mm ni mbavu kuliko wao hapana nilienda na maneno yangu tu wahuni wakamuachia mwamba akanishukuru kwa kunipa tano then akasepa.

Yule mgambo sikumuona tena nahisi alienda kulala kabisa.

All In All Muhuni ni mtu wa ajabu sana.
Nimegoma kuinywa
 
Back
Top Bottom