Wahusika Pigeni Marufuku Makampuni ya kamari kututumia ujumbe mfupi (SMS) kwenye simu zetu

Wahusika Pigeni Marufuku Makampuni ya kamari kututumia ujumbe mfupi (SMS) kwenye simu zetu

Tunzo

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2013
Posts
4,082
Reaction score
2,402
Kama mmepiga marufuku matangazo ya kamari kwenye redio na TV, Pigeni pia marufuku kwenye SIMU.

Ni ngumu kukaa lisaa bila kupokea haya maujumbe (SMS) ya kamari kupitia simu za mkononi, unaweza ukimbilie kufungua simu kuhisi kuna kitu cha maana unakutana na Tangazo la kamari.

Swali lingine ni kwamba je haya makampuni ya simu yanapokea mshiko kiasi gani kutoka kwa makampuni ya kamari kwa kutumia namba zetu kujitangaza?

Na je kama haya makampuni ya kamari wanalipa haya makampuni ya simu kwa kuwapa namba zetu, Gawio la mteja wa simu lipo wapi hapo?

Mimi naamini kama kampuni la kamari liko njema halina haja ya kusumbuka kujitangaza, wateja wanavutana wenyewe, Kuna makampuni yako hapa bongo ambayo hayajawahi hata kutangazwa ila ukifika kwenye vituo vyao watu wamejazana,

Kimbembe cha hizi marufuku kitawakumba wengi makampuni ya kizawa, wanaoishi kiujanja ujanja wajanja.. sijui tano mazuka, sijui buko spot, sijui bum mapesa yani haya yatapata tabu sana. Na yatakayoumia ni yale yanayojitangaza kwa kusema tuma neno flani kwa namba flani kujishinda, haya ndio kwishnei..
Screenshot_20190127-125904_Messages.jpeg
Screenshot_20190127-113918_Messages.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaa eti pesa nyeupe leo, Hivi kweli kuna pesa nyeupe?
 
mie naona sawa tu, sema izo msg waboreshe waruhusu na sie tuwe na uwezo wa kuwajibu waone moto.

Hawawezi kufanya hivyo coz wameshapanga na makampuni ya simu
 
Mkuu unaponunua LINE ya simu soma terms & conditions kwenye kile kikaratasi chao utagundua kuwa wanaruhusiwa kukupa messages za promotions na nyengine kama hizo kwa sababu ile ni line yao wao wanakupa huduma tu, kwa hiyo kuisajili na kuconfirm kuwa umekubali kujiunga nao basi automatically unakuwa umekubaliana na masharti yao.

Halafu hayo makampuni yakubet kama umejiunga nayo kwa line yako ya simu wana masharti yao pia moja wapo ni kukutumia messages zao. Hebu pita upya terms and conditions za mkeka bet au kampuni yoyote ya kubeti uliyojiunga nayo kwa laini yako ya simu utagundua hicho kitu.
 
Mkuu unaponunua LINE ya simu soma terms & conditions kwenye kile kikaratasi chao utagundua kuwa wanaruhusiwa kukupa messages za promotions na nyengine kama hizo kwa sababu ile ni line yao wao wanakupa huduma tu, kwa hiyo kuisajili na kuconfirm kuwa umekubali kujiunga nao basi automatically unakuwa umekubaliana na masharti yao.

Ndio mana nikasema wahusika wapige marufuku na huku, kama wamepega marufuku redioni na kwenye TV wawapige na hawa marufuku hiyo
 
Ukiona hivyo ujue ulishawahi kutumia huduma zao au zinazofanana na hizo sasa ni pale ulipojiunga bila kusoma vigezo na masharti ndo leo unaona usumbufu acheni hizo hyo pia ni biashara na inasomesha na kulisha familia za watanzania, kikubwa tafuta namba za huduma kwa wateja wapigie uwaambie wakutoe kwenye hyo huduma.
Kama mmepiga marufuku matangazo ya kamari kwenye redio na TV, Pigeni pia marufuku kwenye SIMU.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unakuta unatumiwa meseji moja mara 5 kwa siku kila siku kwa makampuni Sita au zaidi utafikiri dose ya mgonjwa wa kifua kikuu
 
Back
Top Bottom