Waifu kanisamehe kikweli kweli au?

cha muhimu elewa jambo ulilomfanyia mkeo sio dogo,wanawake huwa tunaumia sana lakini tunasamehe,na kusamehe kwetu si rahisi kusahau,hebu imagine angekuwa mkeo kakufanyia hivyo si ajabu ungeshalifikisha mbali sana, sasa nakushauri tu uache hiyo tabia muheshimu mkeo na uwe makini na nyendo zako,ila sina uhakika sana kama mkeo kakusamehe mi nadhani kakuweka kapuni tu siku ukilikoroga utaisoma namba mwanawani
 
Anavizia akukate hizo nanhii.....kwa hiyo usilale hata chembe...

japo nimecheka...mie kipindi kile nilimwambia nimemsamehe(na kweli nilimsamehe kuoka moyoni)lakini hakuamni, nilikuwa nikijigeuza anash2ka anajifanya kunywa maji, nikifanya hivi anashtuka, alikuwa halali akihofia nitamfunika na mto ucngizini, alikuwa aapata ucngizi asubuhi mie nikiamka.......mnajitakia matatizo sana nyie.
 

Hio statement umenikumbukusha ofisi moja mdada fulani alikuwa ameolewa kila kukicha alikuwa anamuongelea mume wake na kumsifia jinsi alivyomuaminifu kwake kumbe wanawake wenzake wanamchora na kumcheka tu watu wanamchukulia mumewe kiulani tena hao hao wanawake anaofanya nao kazi ofisini
 

Kusema kweli kama ndo mimi ningezikuta zile sms kwenye simu yake, hakyanani leo ningekuwa mahabusu Keko.
 


kwenye red unamshauri aendelee kufanya lakini aongeze umakini...geez! blue well said, nakuhakikishia kama mwanamke, huyo anafikiria cha kufanya, ogopa mwanamke wa hivyo...utapata kisukari cku hiyo hiyo.
 
thanx me 2.
nikiwekwa kinyumba nitakupa card ya mualiko, nimepotelea ktk maombi ya kukemea roho za nyumba ndogo na aina zote za usaliti ktk ndoa.

Mbona unapemda sana kunipa presha ili mradi tu ujue kama kweli nakupenda, okay haya basi :A S-rose::A S-rose::A S-rose::A S 8::A S 8::A S 8:
 






The Following User Says Thank You to Baba_Enock For This Useful Post:

Asprin (Today)
 
kwenye red unamshauri aendelee kufanya lakini aongeze umakini...geez! blue well said, nakuhakikishia kama mwanamke, huyo anafikiria cha kufanya, ogopa mwanamke wa hivyo...utapata kisukari cku hiyo hiyo.

nyamayao dear u get me wong,i don mean so,what i mean ni kwamba ajirekebishe nyendo zake
 
Jamani hivi wife kanisamehe kikweli kweli au anapanga 'revenge' ambayo nitakiona cha moto?

Ukiona kobe kainama ujue anatunga sheria.

We subili revenge yake lakini usirushe ngumi.
 
So kwenye red hapo unamaanisha kazi za nje niendelee kama kawaida ila niwe makini kwenye sms tu? Asante sana.

hapana,nimeomba uache kuisaliti ndoa yako!
mkeo ni bora kuliko mwanamke mwingine yeyote yule,huko nje huna la zaidi upatalo zaidi ya magonjwa kisha uje umletee na dada wa watu asiye na hatia,mwishowe watoto wabaki yatima.
badili mwendo huo kaka.
 


Duh!, Hayo maneno ni makali sana, yapunguzie kidogo ukali sio wanaume wote wako vile inatokea kwa baadhi, lakini wengine wanaheshimu ndoa zao vilivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…