Waigizaji na filamu za Kenya zilivyojinyakulia tuzo maradufu kwenye Tuzo za Filamu Afrika, AMVCA kule Lagos, Nigeria

hakuna chochote cha maana kwenye filamu bongo...huo ndio ukweli...hasira peleka tandale😀

Kumbe hata huwa unatafuta cha maana humo kwenye filamu za bongo,binafsi sijui kama wakenya wana act filamu.
 
Sasa mkuu unakuta budget $3000 huyo jini akivuka barabara kizembe akagongwa na gari matibabu atalipiwa na nani 😀😀😀 kuwa na huruma na maisha ya jini bwana.
Hahahaaa, Mko na upuzi nyinyi!.. Kwa maswali tuu na majibu nkt, hamjambo!. Hadi mbavu ni uchungu mtupu.
 
Riverwood iko na filamu gani sokoni hapa EA.
Riverwood ni 'film industry' huku Kenya chini ya kampuni nyingi sana za 'production', filamu zao ni nyingi na kuna zile ambazo zimejizolea tuzo nyingi na zikatizamwa kwenye sinema kote duniani, kama 'Nairobi Halflife', 'Veve' na nyingine hiyo iliyoshinda kwenye tuzo za filamu za Afrika 'Supa Modo' imekuwa nominated mwaka huu kwenye tuzo za Oscars kule marekani.
 
Hahahaaa, Mko na upuzi nyinyi!.. Kwa maswali tuu na majibu nkt, hamjambo!. Hadi mbavu ni uchungu mtupu.

Ah tatizo mnakuwaga na upuuzi wa kuanza hivi halafu tunakuja kuwaacha,hamko serious ni kwamba filamu zenu bongo zimeshindwa ushindani au hamjatarget soko hili?
 

Mko na moto ila hamna bahati, hakuna hata filamu moja imeingia Bongo, au mmelenga Wamarekani?
 
Sasa mkuu unakuta budget $3000 huyo jini akivuka barabara kizembe akagongwa na gari matibabu atalipiwa na nani 😀😀😀 kuwa na huruma na maisha ya jini bwana.
Hahaha! [emoji23] Kwahivyo ndio maana jini likivuka barabara huwa linapiga hatua za kweli na za kupasua msamba kama za Idi Amin? Maskini jini, muwe mnalivalisha helmet basi. [emoji38]
 
Ah tatizo mnakuwaga na upuuzi wa kuanza hivi halafu tunakuja kuwaacha,hamko serious ni kwamba filamu zenu bongo zimeshindwa ushindani au hamjatarget soko hili???
Filamu zetu huwa katika lugha mbili (kimombo na kiswahili). Kwa hivyo zile production za Swahili huwa ni lazima zipate ushindani toka za kwenyu ambazo pia hufanywa kwa lugha sawa. Kwa upande unaosalia wa kimombo hapo ni lazima baadhi ya waTZ wasiwe na hamu nazo kisa lugha inawapiga chenga.
 

Bro sisi tunaangali filamu mpaka za kihindi na kifilipino, nini Kiingereza bana!
 
Reactions: Oii
Kumbe hata huwa unatafuta cha maana humo kwenye filamu za bongo,binafsi sijui kama wakenya wana act filamu.
Narudia, hakuna chochote cha maana kwenye filamu za Bongo, na kwa taarifa yako hakuna nchi isiyo na industry ya filamu hata Somalia wanayo.
 
Mkenya Nyce Wanjeri, aliyeshinda tuzo la muigizaji bora wa kike Afrika. Aliwafunika waigizaji wengi sana wa zile filamu za Nigeria za Nollywood, na yale mawigi na makelele yao. [emoji1] Hapo sawa!
Imekuaje.Kenya wawazid ,Nigeria kwa movie industry.tupeane,siri ya mafanikio.
 
Mko na moto ila hamna bahati,hakuna hata filamu moja imeingia bongo,au mmelenga wamarekani???
Kuhusu filamu nyingi za Kenya kutoingia bongo siwezi sema lolote. lakini Kenya wana filamu nyingi tu zipo IMDB. Kitu ambacho kwa Tanzania sijakiona.

Lakini pia nikiwa kama Mtanzania, kwa filamu chache za Kenya ambazo nimezicheck, jamaa wako mbali sana. Kusema ukweli filamu za Bongo nilishaacha kuangalia siku nyingi sana maana hakuna userious wowote.
 
narudia, hakuna chochote cha maana kwenye filamu za bongo...na kwa taarifa yako hakuna nchi isiyo na industry ya filamu hata somalia wanayo...
Lakini ya kwenu hata hapa Arusha hatujawahi kuisikia lakini sidhani wewe kama hujawahi sikia bongomovie?
 
Kenya na filamu wapi na wapi.

Kwenye upande wa filamu, Statistics za mwaka jana ya kwanza ni Nigeria ya pili Ghans, ya tatu ni Tanzania ya nne ni SA. Kenya ipo kwenye mkia.

Mbona mwaka huu tu Monalisa kapokea Tuzo wala hatukupiga kelele. Mwaka jana Lulu kapokea hatujaongea chochote.

Idrisa Sultan kaigiza movie kali ya USA tumekaa kimya tu. Week hii Wema Sepetu kazindua movie inaitwa D.A.D wameshirikiana na Muigizaji bora Africa Toka Ghana. Hiyo movie inapatikana kwenye App ya MPTV mbona sisi tuko kimya tu.
 

Wako mbali ya wapi mzee? Nakwambia hivi, tuna filamu za Kinigeria, Kisouth, Kihindi, Kighana. Zote tunatizama, filamu kuwepo IMDB haimaanishi ni bora, huo ni mfumo tu mzuri industry husika imeuweka kwa maslahi ya wasanii husika.

Labda nikiulize marehem kanumba angeishi hata mpaka mwaka huu,bongo muvie ingekuwa wapi pamoja na ku act mapenzi ya tajiri kumpenda masikini kila siku?
 
Ninazungumzia filamu za Kenya in Relation to Tanzania... Mbna unaenda off topic.... Kuna sehemu nilitaja hizo nchi ulizotaja ww?
 
Ninazungumzia filamu za Kenya in Relation to Tanzania... Mbna unaenda off topic.... Kuna sehemu nilitaja hizo nchi ulizotaja ww?
Hakuna kitu ndugu yangu unachojua kuhusu films industry. Kwa upande wa movie TZ ipo mbele ya Kenya.
Niambie ni movies zipi za kenya na mimi nitakupatia za TZ. Mfano movie ya sumu.
Hebu tazama. Imetengenezwa TZ na Sudan

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…