Ukiangalia waimbaji wa nyimbo za kiimani angalau wakatoliki na wasabato na baadhi ya kwaya kubwa hasa AIC na KKKT.
Nikiangalia hii channel inaitwa Star Religion wanaonyesha nyimbo za injili nagundua...
1: Waimbaji karibu 90% wanajivalia ovyoovyo kana kwamba hakuna mstari wa kimaadili unaowatenganisha na waimbaji wa nyimbo za kidunia. Viduku, suruali zilizochanikachanika, vimini, milegezo.
2: Wengi inaonekana wanaiga nyimbo na mitindo ya nyimbo ambazo sio za dini.
3: Ukimute mtu mwingine akaingia atasema unaangalia Bongoflavour au RnB.
Taratibu mstari unaotenganisha mambo ya kiimani na ya kidunia unaenda unafutika....