Waionaje Kili Stars ya kina Julio/Master?

He! Mkuu, yaani hutaki kabisa kukubali kuwa Boniface Mkwasa"Master" kaku'prove wrong'! Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
Mkwasa namkubali,ila tatizo alikubali 'kukaliwa' na Julio,matokeo akachagua timu mbovu ya wachezaji wengi wa Simba.
 
Kumbe timu ilikuwa hivi! Akh! Lazima watu wazomee. Na nasikia Julio aliwahi kuropoka kwamba Yanga hawachagui kwa kuwa hawana vipaji! Labda amchague Mwape na Asamoah. Kauli na matendo ya Julio pia vili haribu umoja uliotakikana.
 
wachezaji wetu hata pasi hawawezi kupiga! Mashuti hawajajifunza! Samaki mkunje angali mbichi bwana! Zanzibar kwenda Egypt kumewasaidia..umeona pasi,uwezo wa kujiamini wawapo na mpira? Nawaombea siku moja wawe na uwakilishi wa peke yao FIFA!!!! Ikiwezekana sisi ndo tuondolewe.. Kwanza timu yetu haikujulikana ilikuwa ya nchi gani! Jezi za timu zote zilitangaza nchi yao! Kwa maandishi makubwa! Rwanda,Uganda,Zanzibar,n.k. Sisi je?
 
Kumbe timu ilikuwa hivi! Akh! Lazima watu wazomee. Na nasikia Julio aliwahi kuropoka kwamba Yanga hawachagui kwa kuwa hawana vipaji! Labda amchague Mwape na Asamoah. Kauli na matendo ya Julio pia vili haribu umoja uliotakikana.
Kwa kifupi Julio is not national team coach material.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…