Hili ni suala la kisheria. Kwa mujibu wa dini ya kiislam,huwezi kuapa lwa mungu, unathibitisha.
Ndio maana ukiandika kiapo/afdidavit za mahakamani,au ukitakiwa kuapishwa kama shahidi, sheria inasema wakristo wataapa ila waislam watathibitisha. Hii ipo dunia yote.hata ukienda Uingereza utakuta ipo hivyo.
Yaani ukifika pale ukapewa Biblia kama wewe ni mkristo utasema "naapa kwamba....Mungu nisaidie". Ila ukiwa muislam utapewa Quran utanyoosha juu na hutakiwi kuapa kwa quran,unathibitisha,ndio dini inavyosema, utasema " walah bilah wataalah,nathibitisha kwamba...." Hozo ndio aina za viapo kwa wakristo na waislam kisheria.
Usipofanya hivyo,hujaapa kisheria.
Sasa jana Mchengerwa peke yake ambaye ni muislam na anafahamu hili kwasababu amekuwa hakimu kwa muda mrefu huko nyuma,walipompa quan hakusema naapa,alisema nathibitisha. Yeye tu ndio alikuwa sahihi.
Waislam wengine woote waliapa. Sasa swali ni je, kiapo chao ni sahihi? Hao walioapa badala ya kuthibitisha.