Habari Great thinkers
Ninajua kila mtu anaamini dini yake na kuamini kila kitu kipo sahihi kuhusiana na mambo yanayohusu dini yake. Lakini mimi ninasikitishwa sana na kuchokozana baina ya Wakristo na Wailslamu Tanzania. Leo hii ninataka nibainishe mapungufu ya hizi pande mbili kila mmoja achukue nafasi yake kwani bila ya hivyo ipo siku tutajuta na Tanzania haitakalika.
Mapungufu ya Wakristo Tanzania
(1)Wanaamini lazima taasisi au makampuni yote waongoze wao akiongoza Muislam ata taasisi au idara moja kati ya kumi kwao ni shida, wataanza dharau kejeli na underground campaign ata kama anayeongoza ana perform.
(2)Wana maneno ya kejeli kwa Waislam utasikia mara mikanzu yake mara mi kandambili mbaya zaid wanalitumia kwenye kejeli zao jina la Mtume Muhammad bila ya kufikiri ni jinsi gani inawaumiza Waislam hasa hapa JF.
(3)Matajiri, Wafanyabiashara na Waajiri wa Kikristo wana ubaguzi wa wazi katika taasisi ambazo si za dini,mfano Reginald Mengi amewapendelea Wakristo katika ajira na media zake za IPP, kama EATV unaweza zani ni tv ya kanisa kwa kwaya na mambo mengine, mbona hapigi Qasida kila mara kama anavyopiga kwaya.
(4)Siku za hivi karibuni kila kitu wanakitafsiri kwa misingi ya dini.
(5)Wapo viongozi wa zamani na sasa walitumia nafasi yao kudhoofisha Waislam.
(6) Wana ujanja ujanja wa kutumia mali za umma au serekali kusaidia makanisa au ukristo.
Mapungufu ya Waislam
(1)Hawana mipango madhubuti ya kuwaendeleza katika elimu ambayo inaweza wafanya wawe suitable katika usimamizi wa makampuni au taasisi mbali mbali, matokeo wanalazimisha lazima waongoze wao ata kama hawana vigezo.Ninajua wapo wenye vigezo lakini kwa asilimia ndogo ukilinganisha na Wakristo.
(2)Wana maneno ya kejeli na kujiona wao wanajua ustarabu na ubinadamu kuliko wenzao utasikia mara kafiri mara kile mara bwasha.
(3)Matajiri Wafanyabiashara na waajiri Waislam wanaubaguzi wa dhahiri, mfano Bakhresa ameajiri kwa upendeleo kwa Waislam sana kiasi kwamba kuna watu wanabadilisha majina waonekane ni Waislam ili kupata kazi ata ya udereva kwenye kampuni zake, hali hii pia ipo Oilcom kiasi fulani.

(5)Wanaacha na kushabikia baadhi ya watu kama Shehe Ponda wanahubiri chuki na ugomvi baadala ya kushawishi watu wajiunge na Uislam pia uongozi wa Bakwata hauko madhubuti na hawako Tayari kubadilika.
(6) Dunia nzima Waislam ni rahisi kuwagawanya, kuwagombanisha na kuwatumia kwa maslahi binafsi mifano mnayo.
(7) Baadhi ya familia za Kiislam hawako tayari kuingia gharama au kuwa committed ili watoto wao waende mbele Kielimu, ni wazi elimu zote mbili wako nyuma vyuo vikuu vyetu ni wachache na ata elimu ya dini hawapo kwenye mfumo rasmi pamoja na kuwepo na uwezo wakiamua.
(8) Baadhi ni wabishi kila kitu hawataki kutafakari katika mambo yanayotokea.
Jambo baya zaidi katika mambo ambayo Waislam na Wakristo wangeletwa pamoja na Serikali kama miaka michache ya nyuma hali imekua tete kwani wenye madaraka kwenye idara za serikali wameshindwa kuficha hisia zao,na kufanya maamuzi yenye element za udini.
Karibuni wanajukwaa kwa kuchngia ukizingatia malengo Mawili, (1) Dini yako iweze songa mbele na kuwa na nguvu na waumini wengi (2) Tanzania iwe sehemu salama kwa binadamu yeyote ata yule ambaye si wa dini yako. Kubwa zaidi jitahidi kuwa muwazi na mkweli lakini epuka kejeli na dharau kwa mwenzio. Tujadili ili miaka michache ijayo tukiwa kama Nigeria au Misri, tuzisute nafsi zetu.