Walikua walevi ndo maana Nyerere aliwazidi sana calculation
Mpaji...
Soma hayo hapo chini yatakuongezea maarifa katika historia ya uhuru wa Tanganyika:
HISTORIA YA CHIEF DAVID KIDAHA MAKWAIA NA ABDUL SYKES
Kipindi cha uongozi wa Abdul Sykes kati ya 1950 – 1954 hiki kilikuwa kipindi muhimu sana katika historia ya uhuru wa Tanganyika.
Kuanzia mwaka wa 1951 baada ya Gavana Edward Twining kupokea mapendekezo ya katiba kutoka kwa TAA yaliyotayarishwa na TAA Political Subcommitee ambao wajumbe wake walikuwa Dr. Vedasto Kyaruzi, Abdulwahid Sykes, Hamza Mwapachu, Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo, Steven Mhando na John Rupia.
Kamati hii ndiyo iliyokuwa inaweka msingi wa kuundwa kwa TANU wakati ukifika.
Rafiki wa Abdul Sykes Mwanasheria Earle Seaton alikuwa ndiye mshauri mkuu wa TAA katika mambo ya siasa na alisaidia sana katika kuandika yale mapendekezo ya katiba.
Barua za Seaton kwa Abdul Sykes katika miaka ile ni sehemu ya nyaraka nilizosoma wakati wa utafiti na zikaathiri sana fikra zangu.
Katika kipindi hiki ndipo Abdul Sykes akawa na mazungumzo na Chief Kidaha Makwaia kumtaka ajiunge na TAA wamchague kuwa Rais na kisha waunde TANU.
Chief Kidaha alikuwa chief mkubwa sana Usukumani akiwa na machifu 50 chini yake na alikuwa na heshima kubwa kwa serikali ya kikoloni kiasi walimteua kuwa mjumbe wa LEGCO mwaka wa 1945.
Chief Kidaha akiwa na majukumu haya hakuweza kumkubalia Abdul kujiondoa katika uongozi wa watu wake na kujiunga na siasa za TAA.
Historia inaonyesha kuwa kwa kipindi cha takriban miaka mitatu Abdul Sykes hakuitisha mkutano mkuu wa mwaka wa TAA akabakia yeye akiongoza TAA kama Kaimu Rais na Katibu.
Lakini inaelekea Hamza Mwapachu baada ya Abdul kushindwa kumleta Chief Kidaha Makwaia katika uongozi wa TAA, Hamza Mwapachu ndipo alipokuja na jina la Julius Nyerere kuingizwa katika uongozi ule wa juu badala ya Chief Kidaha.
Nyerere mweyewe hakupata hata siku moja kueleza uhusiano wake na Abdul Sykes na Hamza Mwapachu katika kupigania uhuru wa Tanganyika, ukiondoa alipomtaja Abdul Sykes katika hotuba yake ya kuwaaga Wazee wa Dar es Salaam mwaka wa 1985 aliposema kuwa aliyempeleka kwa Abdul Sykes ni Joseph Kasella Bantu.