Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,478
- 3,659
Kwa chama tawala tayari tumeona ndugu Nchimbi yupo pale kuchukua nafasi ya Dkt. Mpango, ambapo Rais aliyepo ni ndugu Samia. Aliyemtangulia ni Hayati Magufuli. Au tuweke hivi;
1. Rais wa kwanza Nyerere - Karume, Jumbe, Mwinyi
2. Rais wa pili Mwinyi -
3. Rais wa tatu Mkapa - Omar, Shein
4. Rais wa nne Kikwete - Shein, Bilal
5. Rais wa tano Magufuli - Samia
6. Rais wa sita Samia - Dr Mpango, Dr Nchimbi
Hapo juu aliyetia doa ni wa awamu ya nne. Sasa tunapokuja kwa upande wa upinzani, tunaenda kushuhudia Mbowe na Lissu wakienda kuchuana kuhusu nani awe mwenyekiti wa CHADEMA. sasa no hivi, kwa mujibu wa takwimu na sera isiyoandikwa kuhusiana na uongozi wa Taifa hili, ni wazi anayekwenda kuwa Mweyekiti wa CHADEMA ni Mbowe.
Kadhalika kama nilivyowahi kuandika awali, na hapa busara itumike sana. Licha ya busara, pia wapo watu nyuma ya pazia wanaopanga karata zao vyema sana. Hivyo basi, akishashinda na kuwa mwenyekiti, nafasi ya kugombea urais atapewa Lissu.
Hivyo basi hali halisi itategemea na upepo utakaokuwepo katika uchaguzi mkuu. Kama Lissu aliweza kumpa tumbo joto Magufuli, ni wazi kwamba Samia atakuwa 'mboga' kwa Lissu. Hapo wafanya maamuzi wa Taifa wataamua kuikabidhi nchi kwa Lissu kama ikibidi. Kama Lissu anataka kugombea urais ni lazima akubali kuukosa uenyekiti. Japo huu ni mtazamo wangu, ndio uhalisia.