Waitara: Duniani kote watakwambia tunapata hasara kwa sababu ndege sio faida moja kwa moja

Waitara: Duniani kote watakwambia tunapata hasara kwa sababu ndege sio faida moja kwa moja

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Leo Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara alikuwa kwenye kipindi cha 'Morning Trumpet' cha Azam TV na amegusia mambo mbalimbali ikiwemo hasara ATCL, ujenzi bandari ya Bagamoyo, ujenzi reli ya SGR na uagizaji wa mabehewa pia ujenzi bwawa la Nyerere
===

Mtangazaji: Umezungumza kuhusu hali ya viwanja vya ndege, vipi kuhusiana na hali ya shirika letu la ndege? Ripoti ya CAG imesema shirika hili limekuwa likiendeshwa kwa hasara na bodi ya wakurugenzi haina wataalam wa masuala ya anga. Mnafanya nini ili shirika la ndege kutengeneza faida au basi kupunguza hasara

Waziri Waitara: Ripoti tuliiona na tuliisoma, tulielekeza wataalam watupe majibu ya zile hoja kabla ya kwenda kwa CAG. Jana nimekaa na watu wa ATCL, tukawaambia mojawapo ya sintafahamu ni jinsi zile ndege zinavyo-operate.

Sisi hatupati faida ya moja kwa moja, vile viwanja vya ndege na ndege zenyewe ni vitu vinavyowezesha lakini wale abiria na hasa watalii wanapoingia, zile shughuli wanazoenda kufanya kule, wamepanda mlima Kilimanjaro, wamelala kwenye mahoteli. Yote yale kwa ujumla ndio unaweza ukajumuisha ile faida, sasa hicho kitu watu wengi hawaelewi, duniani kote watakwambia tunapata hasara kwa sababu ile faida sio ya moja kwa moja.

BWAWA LA NYERERE
Waitara: Huwezi kutaja bwawa la Mwalimu Nyerere bila kumtaja hayati Magufuli na mama Samia mwenye na Majaliwa, hawa ndio viongozi wa nchi ambao walikaa na kuamua.

Mradi huu ulikuwa na makandokando mengi, kwasababu kwanza hawakutaka uanze kabisa, wakasema hii habari ya mazingira lakini kulikuwa na hoja huko nyuma, tukipewa sisi watanzania kuna hoja ya mazingira lakini wakipewa wao wakatekeleza hoja ya mazingira inakufa ndio maana viongozi wakasema hapana, tutumie rasimali ambayo tunayo na unaambiwa hiyo ni asilimia 1, sehemu kubwa zaidi ya asilimia 98 imebaki kuwa hifadhi
 
Bodi haina mtaalam wa mambo ya ndege. Waziri kabisa anasimama na kusema hatuna wataalamu🤣🤣...wtf?
 
Waziri Muongo...Wako wapi hao watalii walioletwa na ATCL?

NA kuna watalii walitaka kuja Tanzania wakakosa ndege?

Je kwa Nini bado flight tickets kushuka Nairobi ni pungufu mara dufu ya Kia?

Kwa Nini bado watalii wanapita Kenya?
 
Bado Magufuli anafanya mambo yake kupitia serikali iliyopo!
 
Haya ndio majibu mepesi kwa maswali magumu. Kwani anakumbuka wakati wananunua ndege shabaha yao ilikuwa nini, ndio kuleta watalii, vipi kuhusu safari za ndani ya nchi?!

Hakuna maendeleo bila ushindani, government ningeona ina nia njema na maendeleo kwenye secta hii kwa kuruhusu uwekezaji. Na hata kuuza hisa baadhi kwa kampuni binafsi kuwezesha hili shilika kufanya kazi kwa ufanisi. Professionalism imepotea.
 
Back
Top Bottom