Waitara nusura atolewe Bungeni kwa kugoma kukaa

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Mbunge wa Tarime Vijijini Mwita Waitara nusura atolewe nje ya ukumbi baada ya kuonyesha kukaidi agizo la Mwenyekiti wa kikao alipomtaka akae chini. Hali hiyo imetokea ndani ya bunge leo Jumatano Novemba 9, 2022 wakati Bunge lilipoketi kama Kamati ya Mipango kwa ajili ya kujadili Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka 2022/23.

Waitara alimaliza muda wake wa kuchangia lakini alipotakiwa kukaa chini aligoma akaendelea kuchangia huku akiwa amezimiwa kipaza sauti. Ni zaidi ya mara sita Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye alikuwa Naibu Spika Mussa Zungu alimkumbusha kukaa lakini aliendelea kuchangia licha ya kuzimwa vipaza sauti.

"Mheshimiwa Waitara kaa chini, kaa chini Waitara, mheshimiwa mbunge muda wako umekwisha kaa chini," alikuwa akisema Zungu. Hali hiyo ilisababisha Askari wa Bunge kusogea eneo la jirani alipokuwa akizungumza Waitara kabla ya kukubali kukaa chini.

Hata hivyo, Zungu alionya kuwa tabia hiyo si nzuri kwa sababu kila mmoja akilazimisha kuzungumza nje ya muda wake haitakuwa jambo jema kwani wengine watakosa kabisa nafasi za kusema. Katika mchango wake Waitara akizungumzia makundi ya watu wasiofanya kazi, michango ya kusaidia kaya masikini (Tasaf) na baadhi ya watumishi kutokuwa waamini katika suala la ukamataji mifugo.

MWANANCHI
 
Wewe mtu umezaliwa mpinzani tangu tumboni halafu unakwenda chama tawala unategemea nini?
 
Kwani hakuna adhabu ya kutandika makofi humo "bungeni"?Angenyukwa makofi hata arobaini tu.
 
Ni Rahisi kumnunua MPINZANI bt nasikitika kusema haiwezekani kununua UPINZANI maana upinzani u katk nafsi.
 
Cha pombe alipenda sana MUJO BAA PALE BUYUNI KUELEKEA CHANIKA KIPINDI HICHO ALIKIA ANAUTWIKA MPAKA ANAANGUSHA TOYOTA
 
Back
Top Bottom