majoto
JF-Expert Member
- Jul 19, 2013
- 2,595
- 4,775
Wandugu tupeane A BC za kumaintain biashara ndogo ndogo ili tuwasaidie wenzetu wanaotaabika na mikopo ya kausha damu. Hapa tuwaongelee wale wajasiliamali wa chini kabisa. Kundi hili linateseka mno mno kwa kujitahidi kujikwamua lakini hawajui jinsi ya kujikwamua.
Nimeumia sana kuna ndugu zangu wanateseka mnoooo na mikopo jamani hadi wanafikia stage ya kujificha au kuhama mtaa usiku kisa kakopa uli aanzishe biashara ya kuuza mbogamboga kabla ya kujua soko na biashara inavyokwenda. Mwingine kakopa ili anunue mfuko wa Azam ngano ili auze maandazi.
Mwingine ndio kaniacha hoi kabisa eti biashara yake ya bagia ilikuwa inaenda vizuri ila kuna mtu jirani anamroga... ukichunguza unagundua anatumia fedha za biashara hadi mitaji inakata deni na riba vinamsonga! Ukimuuliza ilikuwaje hii biashara unaijua... anakujibu niliambiwa inalipa.
Wanawake mtaani wanahaha na mikopo.... akisikia kuna mkopo huku yumo.... anakopa huku analipa huku biashara inakata ili mradi tafrani.