Wajasiriamali jijini Mwanza wanalipia leseni lakini hawapewi leseni

Wajasiriamali jijini Mwanza wanalipia leseni lakini hawapewi leseni

bishoke

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2010
Posts
274
Reaction score
52
Kwa wanajamvi wajasiriamali mlioko jijini Mwanza naomba mnitengulie hiki kitendawili. Kuna jamaa yangu anajaribu kuanzisha biashara jijini Mwanza; tayari kalipia leseni tangu mwanzoni mwa mwezi wa Septemba 2014 lakini mpaka leo ofisi ya biashara ya jiji la Mwanza imeshindwa kumpatia leseni mpya ya biashara kwa kisingizio cha kumaliza vitabu vya leseni.

Je ni kweli kuwa ofisi ya biashara ya jiji la Mwanza inakusanya pesa tu na haitoi leseni kwa kisingizio cha kumaliza vitabu vya leseni za biashara au kuna jambo zaidi ya hilo? Vipi tatizo hili liko Mwanza jiji pekee au na maeneo mengine lipo? Kama lipo je wazoefu huwa mnalitatuaje, kwani ukishalipia pesa zako unatakiwa uanze ujasiriamali mara moja kwani baada ya muda mfupi TRA na jiji hao hao wanataka kodi.
 
Back
Top Bottom