The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Wakati wimbi la mikopo ya kausha damu likiendelea kutikisa nchini, wajasiriamali wilayani Serengeti mkoani Mara wametakiwa kuchangamkia fursa ya mikopo nafuu ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri.
Hayo yamesema na Mwenyekiti Wa UVCCM Mkoa Wa Mara, Mary Joseph wakati akizungumza na wajasiriamali pamoja na kusikiliza kero zao katika Soko la Koreri wilayani humo.
“Wajasiriamali tuchangamkie fursa hii ya mikopo inayotolewa na Serikali ya awamu ya sita, tukiwa katika makundi na kufanya miradi mizuri ili kuhakikisha fedha zitarudi na hatutajiingiza katika mikopo umiza,”amesema Mary.
Pia, katika ziara hiyo Mary amechangia upatikanaji wa mifuko 23 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya UVCCM kata ya Matare, pamoja na kutoa masufuria yenye thamani ya Sh2.5 milioni katika Shule ya Sekondari Koreri ili kuunga mkono ufanikishaji wa upatikanaji na chakula na lishe mashuleni.