Wajasiriamali msaada wako hapa ni muhimu!

Wajasiriamali msaada wako hapa ni muhimu!

goodmother

Senior Member
Joined
Jul 21, 2012
Posts
108
Reaction score
78
Salaam ndugu zangu! Nimekusanya kusanya hatimaye nimefanikiwa kupata kiasi cha Shilingi million kumi (10,000,000) changamoto ni kwamba nataka kuhama mkoa kutokana na familly comflicts. Sasa mawazo yangu ni kuwa nihamie mkoa gani kati ya
Dar na Morogoro? Ukizingatia mawazo yangu zaidi ni kufanya biashara na kilimo cha mboga mboga, kwa kuwa kidogo kilimo cha mbogamboga nina uzoefu nacho,na kuna uwezekano wa kupata shamba Mkuranga kwa msaada wa mjasiriamali wa humu JF. Naombeni mawazo yenu nihamie mkoa gani kati ya hiyo tajwa? Pia sijajua nkifika katika hiyo mikoa nitajishuhulisha na biasharara gani mbali na kilimo. Nb nina watoto wa 4 ambao nitahama nao na siyo mbaya ushauri uzingatie kuwa nina jukumu la malezi ya watoto.
Ushauri jamani na pendekezo la mkoa! Shukrani.
 
We unakimbia famly especial mke, laana yake itakutafuna ts better ukae myamalize, kuhusu mkoa nenda morogoro dsm tumejaaa mkuu pesa inapita kwa wajanja wa fursa,,,hzo pesa kma umezpata kihalali komaa utatoka tuuuu bt dsm kwa 10 m na watoto ts rsk!
 
Moro ni mji mdogo sana kwa mbogamboga. Kwa mbogamboga Dar panafaa na ukaishi maeneo ya Chanika kidogo kuna ustarabu, pia kajishughurishe na ufugaji wa kuku wa asili. ni PM nikuunganishe na jamaa yangu ananyumba Chanika nae tunaishinae huku Biharamulo
 
Soko la uhakika japo bei ndogo ni Dar, masoko ya mbogamboga kwa jumla yapo mpaka mwisho wa mji sehemu kama Gongo la mboto, ukiacha masoko maarufu kama lililokaribu na roundabout ya kigogo.

Kwa ramani ya Dar ya sasa kupata ndani ya mji eneo la kulima ni mtihani, macho yako sana pwani "kisarawe",
Ukiwa karibu na Dar, tuseme Kisarawe, unaweza kusafirisha tenga chache za mbogamboga kitu ambacho ni kigumu ukiwa Moro.
Kwa mtaji uliopo si mdogo kuanzia Biashara, lakini ni Biashara na Maisha, umakini unastahili kupewa kipaumbele.
Jaribu kulima mazao yatakayolipa mapema ukiweka akiba yale yanayochelewa
'mchicha siku 21' ukipanda matuta kadhaa kila wiki inamaana baada ya wiki 3 utaanza kuvuna kila wiki na kupata kipato kwa ajili ya petroli ya w.pump wakati ukisubiri yeboyebo (nyanya chungu), zitakazotoka kabla ya nyanya maji, wakati unasubiri tikiti maji, na wale kuku wakianza kutetea ... nafikiri inawezekana.

Pole kwa yaliyokukuta. Mtangulize Mungu.
Kila la kheri.
 
Mkuu hayo uyasemayo hata hayanihusu, ungenishauri kuhusu swala la namna ya kufanya na hicho kiasi.
 
Mkuu ushauri wako ni mzuri shamba nina uhakika wa kupata mkuranga. Nashukuru nitaufanyia kazi.

E=cha';8233544]Soko la uhakika japo bei ndogo ni Dar, masoko ya mbogamboga kwa jumla yapo mpaka mwisho wa mji sehemu kama Gongo la mboto, ukiacha masoko maarufu kama lililokaribu na roundabout ya kigogo.

Kwa ramani ya Dar ya sasa kupata ndani ya mji eneo la kulima ni mtihani, macho yako sana pwani "kisarawe",
Ukiwa karibu na Dar, tuseme Kisarawe, unaweza kusafirisha tenga chache za mbogamboga kitu ambacho ni kigumu ukiwa Moro.
Kwa mtaji uliopo si mdogo kuanzia Biashara, lakini ni Biashara na Maisha, umakini unastahili kupewa kipaumbele.
Jaribu kulima mazao yatakayolipa mapema ukiweka akiba yale yanayochelewa
'mchicha siku 21' ukipanda matuta kadhaa kila wiki inamaana baada ya wiki 3 utaanza kuvuna kila wiki na kupata kipato kwa ajili ya petroli ya w.pump wakati ukisubiri yeboyebo (nyanya chungu), zitakazotoka kabla ya nyanya maji, wakati unasubiri tikiti maji, na wale kuku wakianza kutetea ... nafikiri inawezekana.

Pole kwa yaliyokukuta. Mtangulize Mungu.
Kila la kheri.[/QUOTE]
 
Dar mzunguko wa fedha ni mkubwa hivyo soko ni kubwa ila uzalishaji gharama kuanzia ardhi na manpower. Ukienda kufanyia nje ya mji kama Mkuranga ni vizuri. Kitu kimoja sijaelewa hii hela ujumuishe malazi na kujikimu wewe na watoto hadi uanze kupata faida au utakuwa na source nyingine? Unategemea kwenda kuishi huko mkuranga au kupata nyumba maeneo jirani mf Chanika? Ni vizuri kuchanganya na mifugo pia maana itakupa mbolea na ni security nzuri ukipata emergency. Mungu akuongoze
Salaam ndugu zangu! Nimekusanya kusanya hatimaye nimefanikiwa kupata kiasi cha Shilingi million kumi (10,000,000) changamoto ni kwamba nataka kuhama mkoa kutokana na familly comflicts. Sasa mawazo yangu ni kuwa nihamie mkoa gani kati ya
Dar na Morogoro? Ukizingatia mawazo yangu zaidi ni kufanya biashara na kilimo cha mboga mboga, kwa kuwa kidogo kilimo cha mbogamboga nina uzoefu nacho,na kuna uwezekano wa kupata shamba Mkuranga kwa msaada wa mjasiriamali wa humu JF. Naombeni mawazo yenu nihamie mkoa gani kati ya hiyo tajwa? Pia sijajua nkifika katika hiyo mikoa nitajishuhulisha na biasharara gani mbali na kilimo. Nb nina watoto wa 4 ambao nitahama nao na siyo mbaya ushauri uzingatie kuwa nina jukumu la malezi ya watoto.
Ushauri jamani na pendekezo la mkoa! Shukrani.
 
We unakimbia famly especial mke, laana yake itakutafuna ts better ukae myamalize, kuhusu mkoa nenda morogoro dsm tumejaaa mkuu pesa inapita kwa wajanja wa fursa,,,hzo pesa kma umezpata kihalali komaa utatoka tuuuu bt dsm kwa 10 m na watoto ts rsk!
Jina lake ni goodmother sasa anakimbiaje mke hapa?
 
Mama joe chanika sipafahamu mpaka nifike huko niangalie na mazingira kama yatafaa kuishi vizuri na watoto yaani siyo uswazi saana mimi popote naishi, ninachoangalia zaidi ni namna gani nitaweza kutumia hicho kiasi na kikazalisha maisha ya kaendelea na watoto wakasoma bila shaka. Nitashukuru kupata washauri kama wewe, pindi nitakapofika dar.
 
Nichangie sifa za Chanika kidogo.

Chanika ni new emerging middle class block kwa sasa. Chanika inakuwa kwa kasi kwa sababu ujenzi wake ni nafuu kidogo as compared na maeneo mengine. Chanika ina mchanganyiko wa watu wa jamii nyingi. Kwa hiyo hata biashara ndogo ndogo kwa Chanika inalipa sana. Wengi wanaohamishwa ktk wilaya ya Ilala wanakimbilia Chanika, kwa sababu ya unafuu wa maisha.

Chongomoto za Chanika ni usafiri saa za jioni, waweza panda magari mpaka manne kwa sababu ya kukata route, miundombinu ya huduma nyingine pia bado kwa kiasi.

Kwa anayehamia Dar na ana kipato cha kawaida sana, Chanika kutamfaa. Sehemu kubwa haijapimwa, kwa hiyo anytime kwaweza kuwa uswahilini.
 
Nashukuru kwa mchanganuo mkuu, sipendi kuishi uswahilini au sehemu ambayo miundo mbinu ni duni sana. Napenda sehemu ambayo kuna usafiri wa uhakika pia huduma muhimu zisiwe mbali. Naona huko chanika hapatanifaa.
 
Mi nakushauri ongozana kina Malila kama unaenda Mkuranga ili kuwa kwenye team inasaidia. Utafanya ukijifunza wenzio wanafanyaje na kuweza share baadhi ya gharama. Itakupunguzia baadhi gharama na hasara kurudia kurudia makosa ya wenzio. Pitia mada uwezavyo jukwaa hili utajifunza mengi sana kuhusu mazao na masoko yake.
 
Mama Joe anajaribu kukushauri kitu muimu sana. Ebu fuata ushauri wake
 
Nitajitahidi kufuata ushairi mama joe. Kweli kuwa kwenye group inasaidia kujua mengi na pia inasaidia kupanua ubongo.
 
Back
Top Bottom