Wajasiriamali wa kitanzania tunakosa uhalisia kwenye suala la bei

Good Father

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2014
Posts
10,321
Reaction score
18,574
Habari zenu wana jukwaa.
Niende kwenye kiini Cha mada, Mimi ni mhangaikaji mwenzenu yaani ni mtu naisaka pesa popote inapopatikana ilimradi iwe njia ya halali.
Natafuta pesa bila kujali ni kazi ya fani yangu au ni kazi yenye hadhi ya chini, nazisaka haswaa, japo sijafanikiwa kimaisha ila naamini nitafanikiwa tu.

Sasa katika hizi biashara zetu sisi wajasiriamali kuna sehemu kubwa tunakosea sana tena sana, Suala la bei za bidhaa au huduma. Tumekua watu wa kutafuta super profit, yaani tuko tayari tuuze bidhaa mwaka mzima kwa Tsh. Laki 5 kuliko kuuza kwa laki 3 ndani ya miezi mitatu au minne.(huu ni mfano tu).

Hivi wapiganaji wenzetu waliokwisha fanikiwa Kama akina Bakhresa leo hii wanauza maandazi ya Tsh 200, sisi wa chini tunajifunza nini? Tuangalie vitu vinavyotaka sokoni kwa uharaka ili biashara isiwe dormant, tuangalie uhalisia wa soko(wateja) Sasa unauza bidhaa uswahilini Cha ajabu unataka kuuza Kama unauza ushuani, utaweza kutoboa kweli?

Tutengeneze vitu au tuuze vitu kulingana na soko Kama Bakhresa na wachina wanavyofanya, tujitahidi kumfikia kila mteja kwa ku-modify ubora na materials zinazotumika kutengeneza bidhaa au kutoa huduma.

Tazameni simu za Tecno zilivyoteka soko hata hapa Tanzania, ivi watanzania wangapi wana uwezo wa kununua iPhone? Sasa wengi wetu hatuna uwezo wa kununua iPhone hapo ndio Tecno wanakomba wateja wa kutosha.

Nitaambatanisha picha hapa chini muone ni kiasi gani tunakosa uhalisia kwenye huduma au bidhaa zetu.

Jiko hilo linatumia mkaa, mtengenezaji anatengeneza kwa gharama ya Tsh. 650,000(laki sita na nusu).
Sasa wewe kama mteja au mtanzania unaweza kukubali kupata huduma hiyo ya jiko la mkaa kwa gharama ya laki sita na nusu?
Je nishati zingine ambazo ni Bora zaidi Kama vile gesi zinaweza kushindana na jiko hili la mkaa?

Huo ni mfano tu, kikubwa tubadili mtazamo wa kutafuta super profit kwenye kila huduma.
 
itakuwa anafanya hivyo kwasababu hana washindani. Hii teknolojia inaitwaje tuigoogle nasisi
 
Kinachosababisha bidhaa kuwa bei juu ni kutokana na ushindani kuwa mdogo kwenye soko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…