Cally30
Member
- Mar 28, 2017
- 5
- 4
Amani ya Mungu iwe nanyi.
Katika kipindi cha miaka mitano hadi sita iliyopita nimeshudia wajasiriamali wadogo( machinga)wakifanya biashara zao maeneo yasiyo rasmi. Baadhi yetu kama wateja limekuwa ni jambo la kufurahisha sana.Kama sio nje ya ofisi, kanisani, msikitini ama shuleni kwako basi hitaji lako litakufwata nyumbani, raha ilioje? Jambo la kusikitisha ni kwamba wajasiriamali hawa wanaathiri maendeleo ya nchi kutokana na sababu zifuatazo:-
(a) Sio walipa kodi.Serikali haiwezi kuwapata kutimiza wajibu huu muhimu.Leo yuko manzese kesho yupo tandale.
(b) Wanadumaza sekta zilizo rasmi.Wanauza dhidhaa zilezile zinazouzwa na wafanyabiashara waliopo kwenye mfumo(wanaolipa kodi) tena kwa bei nafuu kitu ambacho kinawathiri ulipoji kodi wao
(c) Wanadhorotesha,kuzuia ama kuharibu kabisa miundombinu.Watumiaji wengine wa miundombinu wananyimwa haki ya kuitumia ambapo kimsingi ipo kwa ajili yao.
(d) Wanahatarisha usalama.Usalama wa raia unakuwa mdogo.Bidhaa zinapangwa barabarani ivyo barabara kuwa finyu sana
(e) Kuwepo kwa ongezeka la utapeli.Mteja unaweza kuuziwa hata jiwe badala ya kiatu.Muuzaji hana utambulisho na unaweza usikutanenaye milele.
(f) Wamekuwa chanzo kikubwa sana cha uchafuzi wa mazingira na kuharibu madhari ya miji yetu.Kelele kila kona
Kimsingi athari ni nyingi sana kuliko faida yao.Kulingana na utafiti wangu niko na mapendekezo matatu muhimu kutatua changamoto hii.
1: Wajasiriamali hawa kuunda vikundi na kivifanyia usajili.Aidha wanatakiwa wawe na vitambulisho
2: Serikali kutenga maeneo rasmi kwa ajili yao.
3: Serikali na asasi mbalimbali kutoa elimu ya kutosha juu ya umuhimu wa kulipa kodi.
NB: Katika nyakati na maeneo tafauti ya nchi serikali imetenga maeneo kwa ajili ya wajasiriamali wadogo(machinga)bila mafanikio. Hoja kubwa ikisemwa wanawekwa mbali na wananchi kitu ambacho sio kweli. Kuna msemo wa waswahili usemao "wenye shida humumwata mganga"
MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Upvote
0