Wajasiriamali wanaofanya biashara pembezoni mwa msikiti wa Mtoro Kariakoo watimuliwa
Wajasiriamali wanaofanya biashara pembezoni mwa msikiti wa Mtoro wameitaka serikali kuingilia kati mgogoro unaoendelea kati yao na uongozi wa msikiti huo ambapo umewataka wafanyabiashara kuondoka eneo la barabara ambalo wanafanyia biashara kabla na baada ya matengenezo ya barabara.
Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu wa wafanyabiashara hao, Simba Lichanda amesema eneo hilo ndilo wanategemea kufanya biashara ili kutunza familia zao na wapo hapo kwa muda mrefu na viongozi wengi wanaswali na hakukuwahi kuwa na tofauti yoyote walipohitajika kupisha kwa ajili ya shughuli mbalimbali za msikiti huo.