Wajenzi wa nyumba kulipwa tsh 15,000 na vibarua tsh 8,000 kutwa ni sahihi?

Wajenzi wa nyumba kulipwa tsh 15,000 na vibarua tsh 8,000 kutwa ni sahihi?

FrankLutazamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2018
Posts
448
Reaction score
409
Wanatujengea nyumba nzuri sana,wanashinda juani na kula huwa juu yao chai na Chakula cha mchana,watoe humo humo kwenye 15,000 na 8,000,ni sahihi?

Mh.Lukuvi tunakuomba uungurume juu ya hili uwapandishie iwe hata tsh.20,000 kwa Fundi na tsh.10,000 kwa kibarua,nawasilisha.

Instagram jina: kaukwaju
 
Mbona wizara ya ajira ilitoa viwango vya mshahara kwa watumisi wa ndani na madereva

Inatekelezwa?, na kama huna kazi utaacha kuchukua hiyo kdg ufe njaa? vitu vingine ni mpaka soko lenyewe ndiyo inayoamua.nafikiri kila kitu siyo serikali.
 
kunakua na makubaliano kati ya fundi mkuu na mwenyekutaka kujengewa, then fundi ndo atajua awalipe mafundi wenzake kiasi gani na vibarua kiasi gani ili na yeye apate faida. hapo anajua atawabana vipi ili kazi iwahi kuisha na yeye (fundi mkuu) abaki na faida kubwa.
 
Kama ni kampun fundi kuanzia 20+ kibarua 15 hadi 12 lkn kama sio kampun kibarua ni chini ya 10,000
 
LABDA UKO ULIPO WEWE NDIO WANALIPWA HIVYO ILA HUKU MOSHI TUNAJUA KABISA KUTWA YA FUNDI NI 20,000 NA KIBARUA NI 10,000 NA HII ILIANZA SIKU NYINGI SANA SASA NASHANGAA WEWE HUJUI AU MKOA ULIPO NDIO HAWALIPWI HIVYO?
 
Sawa Ila ingekuwa kote huku na sehemu nyingi ni 15 kwa 8
 
Back
Top Bottom