SoC04 Wajibu na haki viendane kwenye kikokotoo cha wastaafu

SoC04 Wajibu na haki viendane kwenye kikokotoo cha wastaafu

Tanzania Tuitakayo competition threads

muda wa ukombozi

Senior Member
Joined
Jun 28, 2013
Posts
129
Reaction score
118
Bunge ni chombo muhimu sana kwenye nchi yoyote, na ndicho chombo chenye dhamana ya kutunga na kupitisha sheria mbalimbali katika nchi husika.

Hapa kwetu Tanzania kuna mabunge mawili la Tanzania Bara na la Zanzibar kwa wakati tofauti mabunge haya yamepitisha sheria mbalimbali, lakini sheria hizo hazina haki na wajibu kwa kila Mtanzania, kwa mfano kuna sheria iliyoruhusu mifuko ya kijamii PSSSF na NSSSF kuwakata wastaafu zaidi ya 50% ya mafao yao wakati wanastaafu, haya ni mabadiriko yaliyopitishwa na bunge, sababu ni nyingi ikiwemo kwamba mstaafu akipewa yote ataimaliza mapema na kusababisha maisha yake yawe ya taabu, lakini kama ni kweli mstaafu wa kitanzania anastaafu akiwa na miaka 60, alafu anakuja kufariki akiwa na miaka 70 hizo fedha anapewa nani? Ule utaratibu wa pensheni ya kila mwezi na mstaafu alikuwa anapewa kiinua mgongo chake chote kilikuwa na madhara gani?

Nilikuwa naomba Serikali yetu sikivu ikae chini tena kuchakata hii sheria aidha ifanyiwe marekebisho ioneshe kwamba ni kweli hii hela imetunzwa na ijulikane ni shilingi ngapi na ikitokea mstaafu amekufa ieleze hiyo hela ataendelea kupewa nani hadi iishe yote au turudi kwenye mfumo uleule mstaafu apewe chake chote na kila mwezi apewe pensheni yake kwasababu hiI ya sasa haioneshi hiki anachopewa kwa mwezi ni sehemu ya kiinua mgongo chake au ni pensheni?

Hapa kuna tatizo kubwa sana kati ya Serikali na wastaafu kuna jambo halijakaa sawa kuna fedha nyingi za wastaafu hazielezeki, utakuta mstaafu alipaswa alipwe kiinua mgongo Milioni 100, kwa sheria hii anaweza kupata kwa mfano Milioni 30, alafu anakuja kufa baada ya miaka mitatu hizo fedha zote hazi saidii mazishi na hata tegemezi waliobaki (flew away).

Madhumuni ya mabadiriko haya hayana mashiko kwa watumishi wa umma zaidi baada ya hili kuanza kazi serikali imetengenexa wasiwasi kwa watumishi wa umma, watumishi wa umma wenye tatizo la afya akili wameongezeka, ubora kwa huduma kwa wateja unapungua kila mtumishi anapokaribia ku kukokotolewa.

Cha kushangaza waliotunga sheria hiyo wao kikokotoo hawakiwahusu, mawaziri hakiwahusu, wasimamizi wa fedha Benki Kuu hakiwahusu, Wanajeshi hakiwahusu, kinawahusu taasisi zingine zingine tu ambazo ata zikipiga kelele hazisikilizwi zaidi ya kupigwa spana, kuwe haki na wajibu katika kutekeleza sheria zinazotungwa na Bunge, hiki kikokotoo kiwe kwa wote na sheria itamke hivyo kuanzia mtumishi namba moja namaanisha Rais hadi mtumishi wa mwisho kabisa kwa mujibu wa utaratibu, kwa jinsi ilivyo sasa ni kuonea watumishi wachache wasio kuwa na sauti, kupitia hii platform ya stories of change ningependa utawala mpya utakaoanza 2025 ungerudisha siha na afya ya akili kwa watumishi wa umma kwa kuondoa kabisa kikokotoo isiwe kama hivi double standard.

Napenda kuweka kalamu chini na kutamatisha. Ahanteni sana.
 
Upvote 5
mifuko ya hifadhi ya jamii haina pesa. ccm inazichota na kuzitapanya hovyo.
 
Back
Top Bottom