Dr James G
Senior Member
- Oct 16, 2016
- 158
- 267
Utangulizi
Bima ya afya ni huduma ya mafao ya faida ya mfuko wa afya unao mrahisishia mteja kupewa huduma za kimatibabu wakati wowote anapohitaji huduma hiyo.
Miongoni mwa huduma ambazo wateja wa huduma za afya wananufaika nazo ni huduma ya kumuona daktari ,gharama za vipimo,gharama za Dawa,huduma za afya ya tiba ya kinywa na meno,pamoja na upasuaji mdogo na mkubwa.
Kuna aina tofauti za bima ya afya zinazopatikana nchini kwetu kama vile
National health insurance fund (NHIF) hii ni bima ya afya ya taifa iliyoanzishwa chini ya sheria ya bunge ya the act of parliament no 8 ya mwaka 1999 na kuanza kutumika mwaka 2001,mwanzoni bima hii ilikua kwa ajili ya watumishi wa umma tu lakini sasa hivi hata wasio watumishi wa umma wanaweza kutumia bima hii .
#picha kutoka kurasa ya NHIF
community health fund(CHF), hii bima ililenga zaidi jamii kiujumla na zaidi vijijiji na watu Wenye kipato kidogo na sio lazima kujiunga ilikua ni uchaguzi tofauti na bima ambazo ukijairiwa unakatwa moja kwa moja.
Mbali na kua na umuhimu wa Bima ya afya lakini ni idadi ndogo sana ya watu ambao wanakadiriwa kua na bima ya afya ,kwani ni asilimia 15 tu ya watu waliojiunga kua na bima ya afya uku asilimia 99 wakijiunga wakati wakiwa wagonjwa.
Ukosefu wa elimu ya kutosha kwa jamii juu ya faida za bima ya afya, umasikini wa kushindwa kumudu kuchangia bima ya afya,ukosefu wa ajira Rasmi, kipato kidogo kwa ajira zisizo rasmi vimechangia kiasi kikubwa cha watu wengi kutojiandikisha na mifuko ya bima ya afya.
Faida kubwa ya kua na bima ya afya ni kupunguza matumizi Makubwa ya hela Pindi unapougua gafla au kuuguliwa na watu wako wa karibu ,kukosa hela ya matibabu wakati wa magonjwa ya dharura na kushindwa kupata huduma za matibabu kwa wakati.
Ni kweli kua palipo na faida hapakosi changamoto na changamoto nyingi zinazojitokeza katika mifuko ya bima ya afya imekua chanzo cha wateja wengi kukata tamaa na huduma ya bima na kupeleka kutibiwa kwa hela mkononi wakati bado anakatwa bima kila mwisho wa mwezi ,tatizo hili limekua ni chanzo cha migogoro Mingi wakati wa kutoa huduma kwa wateja wa bima za afya ,miongoni mwa changamoto hizo ni ukosefu wa Dawa husikia kwa wagonjwa,Bima kushindwa kuhudumia baadhi ya magonjwa sugu au magonjwa ya muda mrefu ,hospitali kucheleweshewa Malipo ya kutoa huduma kwa wateja wa bima ya afya hivyo kupeleka kuwapa kipaumbele wagonjwa wanaolipa hapo,changamoto hizi zimekua zikisababisha migogoro inayorudisha nyuma utekelezaji wa Malengo haya mazuri ya kumsaidia mnufaika wa bima kua na uhakika wa matibabu wakati wote,
Changamoto katika mifumo ya wasimamizi wa huduma hii umekua haufuati utaratibu wa huduma bora na uwajibikaji kwa wateja,na kusababisha uvunjifu wa uaminifu kwa watoa huduma za afya na wagonjwa au wateja wao.
MUSWADA WA BIMA YA AFYA KWA WOTE (UHC)
Kwa miaka 3 sasa serikali kupitia wizara ya afya ilianzisha mjadala wa kupitisha muswada wa bima ya afya kwa wote ,muswada ambao hadi sasa bado haujafanikiwa kupita bungeni ili kua sheria na kutumika kwa wananchi.
Ni ukweli usiopingika kua kuna umuhimu mkubwa sana kua na bima ya afya kwa binadamu wote kwani itasaidia kupunguza gharama za matibabu wakati huduma ya dharura inapotokea.
Lengo la wizara kuja na bima ya afya kwa wote ni kuhakikisha tunachangina huduma za matibabu na kuongeza wigo wa kupata uhakika wa matibabu kabla ya kuugua , wazo Lao kubwa ni kufungamanisha na baadhi ya huduma Zingine za kijamii bila kujali hali ya kipato ya mgonjwa kwa wakati huo.
Miongoni mwa huduma zinazopendekezwa katika bima ya afya kwa wote ni Ada ya kuandikishwa na kumuona daktari,gharama za Dawa,vipimo na Kulazwa,gharama za upasuaji mdogo na mkubwa,gharama za matibabu Bingwa na upasuaji unaofanywa na madaktari Bingwa ,huduma za matibabu ya macho ,afya ya kichwa na meno,Vifaa vya kufanyia mazoezi ya viungo na vifaa tiba saidizi.
KWANINI MUSWADA HUU UMECHUKUA MUDA MREFU KUA SHERIA?.
Mbali na mazuri mengi yanayoonekana katika muswada wa bima ya afya kwa wote lakini bado kumekua na changamoto juu ya utekelezaji wake kwa wananchi ,kwanza kabisa ushirikishwaji kwa wanachi na wadau wa afya umeoneka kua mdogo sambamba na jamii kutopata elimu ya kutosha.
Mbali na kutokuepo kwa elimu ya kutosha na ushirikishwaji lakini pia muswada huu unaonekana kutokua endelevu zaidi kwa watu Wenye kipato cha chini kabisa,kwani serikali haijabainisha vyanzo vingine vya kugharamia matibabu hayo kwa watu wa hali ya chini.
Pia muswada ulikua unanyima watu wengine huduma hiyo kwa kutokua na kadi ya Utambulisho wa taifa ya NIDA,kwa sababu sheria inataka ili uwe Mwanachama wa bima ya afya lazima uwe na kadi ya NIDA kwa maana hivyo sheria isingeweza kutekelezeka kwa wote.
Muswada haujabainisha mtu asiye na kipato ni yupi na chanzo ya Kipato kwa mtu huyo kitakua kipi ili kugharamia matibabu yake.
Mapungufu kwa watoa huduma za afya kwa sifa za mtoa huduma anayeweza kumhudumia mgonjwa na kujaza form ya mgonjwa .
NINI KiFANYIKE
Serikali kupitia wizara ya afya Inawajibu wa kutoa elimu ya kutosha kwa Jamii pamoja na ushirikishwaji wa wadau mbalimbaili.
Kuhainisha vyanzo vya mapato kwa watu wasio na uhakika wa kugharamia matibabu hayo mfano serikali inaweza kuanzisha chanzo endelevu kutokana ongezeko la thamani yaani VAT kwa kuwasaidia wasio na kipato cha kugharamia matibabu.
Kuimarisha huduma katika ngazi zote za kutolea huduma za afya mfano kuanzia kwa watoa huduma za jamii,Zahanati ,vituo vya afya hadi hospital za Rufaa.uimarishaji wa huduma hizo uendane na kubainisha uhakika wa huduma zote muhimu kwa ngazi husika kwa kufanyia kazi mapungufu yaliyopo sasa mfano upungufu wa Dawa na vifaa tiba kwa wagonjwa wanaolipia huduma za bima ya afya.

Upvote
19