Pre GE2025 Wajibu Wa Vyombo vya Habari katika Uchaguzi

Pre GE2025 Wajibu Wa Vyombo vya Habari katika Uchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Dalton elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
373
Reaction score
829
Vyombo vya habari vina wajibu mkubwa wa kuripoti kwa umakini na usahihi habari mbalimbali hasa zinazohusu uchaguzi ili kuipa jamii kile ambacho inachostahili.

Wakati wa kampeni waandishi wa habari wana wajibu wa kutopendelea vyama vya siasa kwa kuegemea kuripoti habari za chama fulani na kuacha wagombea wengine wakishindwa kuripotiwa habari zao,” anasema Kiondo Mshana na kuongeza wakati wa kampeni wagombea wanatakiwa kuwa huru kunadi sera zao pamoja na kuendesha mikutano yao bila kuingiliwa.

wanahabari wanapaswa kufuatilia kwa karibu kura zilizohesabiwa vituoni kuanzia mwanzo wa upigaji kura hadi siku matokeo yanapotangazwa kama njia ya kuiwezesha jamii kupata habari zauchaguzi kwa usahihi na kwa wakati.

Soma Pia: Waziri Mchengerwa: Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Bara utafanyika 27 November, 2024

Pia wanatakiwa kuzijua sheria za uchaguzi, pia waepuke ushabiki kutoa hitimisho wakati wa kuripoti habari hizo hasa wanapogundua chama fulani kimeshinda. Mengine ya kuzingatia ni kuepuka kuandika habari za uchochezi.

Tukiripoti habari za uchaguzi bila kujua idadi ya wagombea, kilichotokea katika chaguzi zilizopita nakadhalika. Cha msingi tunachopaswa kuzingatia ni kuepuka ushabiki bali kunatakiwa kuripoti kwa usahihi habari za uchaguzi.
 
Back
Top Bottom