Wajinga ndiyo waliwao

Wajinga ndiyo waliwao

feyzal

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2016
Posts
7,683
Reaction score
15,128
Nikiwa kwenye harakati zangu za kimaisha, jana nikapita pale Mbagala Rangi Tatu kumsalimia jamaa yangu muuza nguo za akina dada za ndani (vifuniko vya asali).

Karibu na eneo analopigia biashara kuna biashara zingine ila kuna jambo likanivutia zaidi ilikua hivi.

Kuna mnada wa nguo na vitu mbalimbali kama mabegi, kanga, shati nk. Sasa jamaa yuko juu ya kizimba anatangaza shati kali 500 mara ya kwanza mara 1000 mara ya pili wanaenda mpaka elfu 10 anauziwa mtu, anachukua tena begi begi elfu 3 anakwenda hadi elfu 8 begi jipya ananunua mtu.

Nikasema alaa mbona bei mtelezo, jamaa angu akacheka akasema ndugu usithubutu hata kusogea pale wale wote waliopewa vizuri ni wenzao na subiri uone mtu anavyolizwa na wakikuhisi mjanja wanakuondoa. Hebu angalia pembeni unamuona huyo muuza mihogo? Sasa subiri kidogo afu nenda pale kwenye mihogo fanya kama unanunua jitahidi uchungulie kwenye kibanda chake utaona walionunua wanarudisha vitu pale nyuma vinachukuliwa tena vinauzwa tena kwa wale wale kuvutia watu.

Basi bwana akaja mama mmoja na yeye akavutiwa zikatolewa kanga na vitenge zikatangazwa pale basi wakapelekana na washindani hadi elfu 8 akarushiwa, salale!! baada ya kudaka ile kanga hata 500 asingetoa akataka kuleta shida akatulizwa na watu, simple akaondoka huku amefura kwa hasira, mchezo uliendelea tena na tena. Ajabu wanunuzi wengine waliokua wananunua vitu vizuri vizuri wanaondoka na mizigo na wanarudi hawana mizigo kumbe wanapeleka kwenye kile kibanda.

WAJINGA WALI WAO TUSIPENDE URAHISI JAMANI MTAPIGWA.
 
98c6c6127478471.614289d58eeaf.jpg
 
Nikiwa kwenye harakati zangu za kimaisha, jana nikapita pale Mbagala Rangi Tatu kumsalimia jamaa yangu muuza nguo za akina dada za ndani (vifuniko vya asali).

Karibu na eneo analopigia biashara kuna biashara zingine ila kuna jambo likanivutia zaidi ilikua hivi.

Kuna mnada wa nguo na vitu mbalimbali kama mabegi, kanga, shati nk. Sasa jamaa yuko juu ya kizimba anatangaza shati kali 500 mara ya kwanza mara 1000 mara ya pili wanaenda mpaka elfu 10 anauziwa mtu, anachukua tena begi begi elfu 3 anakwenda hadi elfu 8 begi jipya ananunua mtu.

Nikasema alaa mbona bei mtelezo, jamaa angu akacheka akasema ndugu usithubutu hata kusogea pale wale wote waliopewa vizuri ni wenzao na subiri uone mtu anavyolizwa na wakikuhisi mjanja wanakuondoa. Hebu angalia pembeni unamuona huyo muuza mihogo? Sasa subiri kidogo afu nenda pale kwenye mihogo fanya kama unanunua jitahidi uchungulie kwenye kibanda chake utaona walionunua wanarudisha vitu pale nyuma vinachukuliwa tena vinauzwa tena kwa wale wale kuvutia watu.

Basi bwana akaja mama mmoja na yeye akavutiwa zikatolewa kanga na vitenge zikatangazwa pale basi wakapelekana na washindani hadi elfu 8 akarushiwa salale baada ya kudaka ile kanga hata 500 asingetoa akataka kuleta shida akatulizwa na watu, simple akaondoka huku amefura kwa hasira, mchezo uliendelea tena na tena. Ajabu wanunuzi wengine waliokua wananunua vitu vizuri vizuri wanaondoka na mizigo na wanarudi hawana mizigo kumbe wanapeleka kwenye kile kibanda.

WAJINGA WALIOWAO TUSIPENDE URAHISI JAMANI MTAPIGWA.
Hapo mwishoni sijakuelewa
 
Nishawahi kununua simu elfu 10 kwa hao jamaa
 
yaani hapa bongo ukiona unaitiwa fulsaaaaa......................
 
Back
Top Bottom