Wajua japo Rais ni sehemu ya Bunge, bado hana mamlaka ya kuliingilia Bunge? Ili kufuta IGA ya DPW, Rais anapaswa kulivunja Bunge?

Toka umepewa rushwa ya kutangaza channel 10 umekuwa mtu wa hovyo sn, kwanza hatuna bunge tuna genge la matapeli pale na majangili, pili TEC hawajaanza kutoa waraka leo hata kipindi cha dikteta walitoa na ni mkatoliki mzuri sn, TEC kazi yao ni kusimamia maslahi ya taifa na siyo kuwa chawa wa CCM kama ilivyo BAKWATA.
 
Hiyu ana maslahi binafsi na hili jambo,si kama anavyojipambanua eti "...kwa maslahi ya taifa..."
 
Unapojitambulisha kama Mwandishi au Mwanasheria, basi Jifunze kuandika kama Mwandishi au Mwanasheria. Siyo kuja na maandishi mareefu ya mipasho kama wimbo wa Tupac uitwao "Hit em up".

Kwa ushauri tu, unapoandika kwamba 'Maaskofu wamesema' basi jitahidi ku quote hiyo statement. Maana hiyo tabia ya kujitafsiria mtakavyo ndiyo baada ya hatua mbili mbele mnakuta mmeshahamisha mjadala wote na kuleta kitu kipya kabisa ambacho wala hakipo.
Waraka umeshauri, hamtaki ku quote ushauri na badala yake mpo busy kusambaza parenthless and bracketed words badala ya words in single and double inverted commas.

Pathetic!
 
Kumbe maaskofu wetu hawaijui katiba!, hawajui kuwa kwa mujibu wa katiba yetu, Rais wa JMT hana mamlaka ya kufuta Azimio la Bunge!, ili Rais Samia alifute Azimio la Bunge, inambidi Rais Samia alivunje Bunge!.
Kusitisha wasilisho la azimio la Bunge ni sawa na kufuta azimio la Bunge?
 
Kilifanyika, mbona Kiko wazi
Mayala rafiki yangu ni kweli kuna mihimili mitatu, yahani , Sarikali,Bunge na mahakama. Hii kwa tanzania ndiyo lakini inabakia kwenye kitabu cha katiba. Kwenye utendaji tanzania ina muhimili mmoja na vivuli vya mihimili miwili. Namaanisha kuwa tuna muhimili wa Serikali na vivuli vyake yahani Bunge na Mahakama. Naomba ufikilie vzr Muhimili wa Bunge la tanzania unapatikanaje. Wabunge wetu hawaingii bungeni kwa kura za wanajimbo Wanasaidiwa na Serikali kuwa wabunge (wanawekwa) kwa sababu hiyo ndiyo unaona wanafanya kazi moja kati ya tatu za kikatiba. Yaani ,kupitisha miswada ili iwe sheria. Badala ya kutunga sheria.Kuishauli Serikali ili wanalifanya na la kuisimamia seikali alifanyiki kabisa. Naomba nikukumbushe kauli ya rais Magufuli kwa mihimili hii miwili. Naanza na bunge, Ninani ameingia humu kwa kushinda wabunge wote kimya. Mahakama , Mnasema mihimili yote hiko sawa wewe jaji ni nani anatoa pesa , serkali ama bunge?. Ni kauli za Magufuli. Kwetu tanzania rais ndiye kila kitu mayalla naamini unajua ila unajisahaulisha tu
 
Paskali bana, kwa hiyo unatarajia Rais atoe tamko? Yeye anampa maelekezo spika, baraza la mawaziri mchakato unaendelea.
 
Na huu utamaduni kwamba mtu anawatia msala wa maisha halafu adhabu yake iwe kuishia 2025 ifike mahali ukome.

Mtu wa namna hii katika mataifa serious ananyooshwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu P. Pia bunge lingeukataa mkataba Rais pia angevunja bunge. Kwaheri
 
Unafiki pembeni.

Hilo kundi lililomo kwenye ukumbi wa bunge silichukulii kuwa lapaswa kuitwa wabunge kwa mtazamo wangu.

Ndio maana sishangai kwa maamuzi wanayoyapitisha ,wewe ni shahidi hiki kikundi kilipatikanaje mwezi October 2020 japo hadi leo huwa haukubali sababu ni kada unasema "zilikua dosari ndogo ndogo"

Mwisho nihitimishe kwa kua kundi hili 98% liliingia kwa by hooks or by crooks bunge halitakua dissolved kirahisi kabisa usitegemee ukijumlisha na hakuna pure " check and balances" rejea lile jibu la mhimili uliojichimbia chini zaidi utabaki kuona kuwa utalindwa na hili kundi hata iweje na hili kundi tukiitisha uchaguzi huru kwa sasa hata 5 % hawatorudi ukumbini.

Sina imani hata 0.000001% kwa hili kundi (Mimi kwangu halina hadhi ya kuitwa bunge)
 
Mkuu hapa linazungumziwa BUNGE au BINGE? Maana umerudia mara nyingi
 
Kama aliweza kumtoa Spika wa Bunge na maisha yakaendelea, akamuongezea Jaji mkuu mda kinyume ba katiba na maisha yapo yanaendelea. Hayo makaratasi ndiyo yamshinde. We mzee nawe unazeeka vibaya ujue!
DP W for better TZ
 
Ikiwa Bunge hawawezi kufanya marekebisho au kuufuta kama walivyo shauriwa baada ya kuupitisha, na Raisi hawezi kuuingilia Mihimili mwingine bila kuvunja Bunge, basi na iwe hivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…