Wajue: Baadhi ya wanawake waliosaidia katika ukuaji wa sayansi na Teknolojia.

Wajue: Baadhi ya wanawake waliosaidia katika ukuaji wa sayansi na Teknolojia.

I am Groot

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2018
Posts
3,929
Reaction score
10,747
1. Katherine Johnson (1918-2020)
Katherine-Johnson.jpg

Picha Credit: Alex Wong /Getty Images​

Katherine Johnson alikuwa mwanamke mwanahisabati na mmoja wa wanawake wa kwanza wenye asili ya African-American kufanya kazi kama mwanasayansi chini ya kampuni ya NASA. Kama mwanahisabati, alifanikisha kukokotoa na kuchambua njia ya chombo cha anga cha NASA.

::Anajulikana sana kwa mahesabu yake yaliyofanikisha wamarekani wa kwanza kufika katika mzingo wa dunia na kuweka nyayo mwezini.

~Mwaka 2016 ilitengenezwa movie ya maisha yake na safari yake ya kisayansi chini ya NASA yenye jina" HIDDEN FIGURED"

2. Marie Curie (1867-1934)
Marie-Curie.jpg

Picha Credit: Hulton Archive /Getty Images​

Marie Curie alikuwa mwanafizikia na mkemia aliyefanya utafiti mkubwa wa tabia za mionzi. Aligundua chembe aina mbili mpya za kikemikali: radium na Polonium. Curie aliongoza project ya kwanza ya kiutafiti katika uwezekano wa utabibu wa (vimbe-Tumors) kwa njia ya mionzi.

Pia aliwekeza nguvu kwenye taasisi yake - kwa sasa inajulikana kama (the Radium Institute)- ambayo inajikita katika utafiti wa madawa kule Paris, France, ikitilia mkazo katika utafiti wa cancer na tiba ya mionzi. Curie alikuwa mwanamke wa kwanza kushinda tuzo za NOBLE PRIZE mara mbili.

3. Valentina Tereshkova (1937)
Valentina-Tereshkova.jpg

Picha Credit: David M. Benett / Getty Images Europe​

Valentina Tereshkova ni mwanainginia, na alikuwa mmoja wa wawakilishi wa bunge huko Russia, na mwana anga za mbali wa Soviet aliyestaafu. Mwaka 1963, June 13; alikuwa mwanamke wa kwanza kusafiri kwenda anga za mbali (space). Aliizunguka dunia mara 48 kwa siku 3 tu.

Baadae aliingia kuwa member wa chama cha kikomunist na kuiwakilisha USSR katika majukwaa mbalimbali ya kimataifa. Tereshkova amebaki kuwa mwanamke pekee kuwahi kupewa mission ya peke yake kwenda space!

4. Elizabeth Garrett Anderson (1836-1917)
Elizabeth-Anderson.jpg

Picha Credit: Hulton Archive /Getty Images​

Elizabeth Garrett Anderson alinyoosha njia ya wanawake katika madawa huko Britain kuu (Uk). Alikuwa dokta wa kwanza wa kike England na kuvishinda vikwazi vingi alivyokutana navyo miaka hiyo ili kufanikisha kuwa professional katika kipindi ambapo mwanamke hakuruhusiwa kujihusisha na mambo ya madawa.

Alifungua Shule ya Madawa huko Britain kuu. Na alikuwa mwanamke wa kwanza kuongoza shule ya madawa na mwanamke wa kwanza kuwa mayor England.

5. Chien-Shiung Wu (1912-1997)
Chien-Shiung-Wu-.jpg

Picha Credit: Bettmann / Getty Images​

Chien-Shiung Wu alikuwa kiongozi na mwanzilishi katika nyanja ya physics. Akiwa kama mwamiaji wa kichina huko United States, Wu alikuwa mwanamke wa kwanza kuajiriwa kwenye idara ya physics katika chuo cha Princeton.

Baadae alihamia kikazi kwenye chuo cha Columbia kujiunga na project Matthan- iliyoleta matokeo ya uundwaji wa silaha za nyuklia. Anajulikana kwa kutoa ushahidi kwamba "the identical particles do not always behave in the same manner"

Alipewa tuzo ya Wolf prize in physics mwaka 1978 na nickname "the lady of physics".

6. Rosalind Franklin (1920-1958)
Rosalind-Franklin.jpg

Picha Credit: Donaldson Collection/ Getty Images​

Rosalind Franklin Alikuwa mkemia wa kibritish. Anajulikana kwa uvumbuzi wake wa molecular structures za DNA, RNA, Viruses, Makaa ya Mawe, na graphite.

Kwa kutumia teknolojia inayoitwa X-ray crystallography, aligundua umbo la shape ya DNA.

7. Ada Lovelace (1815-1852)
Ada-Lovelace.jpg

Picha Credit: Hulton Archive / Getty Images​

Ada Lovelace anachukuliwa kama mmoja wa maprograma wa kwanza wa kompyuta duniani. Mwaka 1880's kabla kabisa hata ya kompyuta kugunduliwa- alisaidia kuibua idea kutengeneza mashine (kompyuta). Alibuni algorithm ambayo ingeweza kufanikisha lengo hilo.

Ili kuenzi mchango wake, idara ya usalama ya marekani iliamua kuipa jina lugha mpya ya Computer "Ada" miaka ya 1990's.

8. Sally Ride (1951-2012)
Sally-Ride.jpg

Picha Credit: Orlando Sentinel / Getty Images​

Sally Ride alikuwa chachu kwa wanawake na mabinti katika elimu ya sayansi na hisabati. Kama mwana anga (Astronaut), alikuwa mwanamke wa kwanza marekani kufika anga la juu mwaka 1983. Kwenye mission ya 2 na ya 3 ya chombo anga cha NASA, kazi yake ilikuwa kukontro mikono ya robot iliyotumia kuweka satelite kwenye space.

Baada ya kuacha kazi NASA , alianzisha NASA's Earthkam project, ambayo ilisaidia wanafunzi kupata picha za dunia na kujifunzia nazo.

9. Marie-Anne Paulze Lavoisier (1758-1836)
Marie-Anne-Paulze-Lavoisier.jpg

Picha Credit: Picturenow / Universal Images Group / Getty Images​

Marie-Ann Paulze Lavoisier anatambuliwa kama mama wa kemia ya kisasa. Alikuwa mke wa mkemia na mtu mashuhuli Antonie Lavoisier, na kama msaidizi wa mahabara.

Marie-Anne aliongea kifasaha lugha ya kilatini, English na kifaransa, alimsaidia sana mme wake kutafsiri kazi kadhaa za kisayansi. Tafsiri hizo za Lavoisier zilipelekea ugunduzi wa gas ya Oxygen. Pia alikuwa kama chombo cha usawa katika mambo ya kisayansi.

Leo hii, vyuo vingi vinania ya kutengeneza ongezeko kubwa la ushiriki wa wanawake katika sayansi, teknolojia, inginia, na hisabati (STEM).
 
Catherine Johnson amestahili kuwa number moja hapo. She was like computer inserted in her brain.
Hata hivyo tungepata na list ya Africans walio ndani ya Africa pia.
 
Back
Top Bottom