Ngufumu
Member
- Dec 29, 2016
- 25
- 44
Anaemia/ Upungufu wa Damu kwa wajawazito
Je unajua upungufu wa damu huchangia 14.5% ya vifo vya kinamama(Martenal Deaths) Tanzania?
Kiasi cha damu pungufu ya 11g/dl uhesabika upungufu wa damu kwa Mjamzito ambapo kikawaida hutakiwa kuwa 11.5 - 13g/dl wakati huu
Fuatana nami sasa 👇🏿
Upungufu wa damu ni moja ya tatizo linalopelekea Watu(general population siyo wajawazito tu) kulazwa hospitali, ikishika nafasi ya 4 kwa magonjwa ya kulazwa ambapo kwa kipindi cha 2023/2024 Watu 29,913 sawa na 8.72% ya wagonjwa waliolazwa Tanzania walikuwa na Upungufu wa Damu
Tukirudi kwa wajawazito na wanawake inakadiriwa na Shirika la Afya Duniani(WHO) kwamba 38% ya wanawake wote wajawazito(Duniani) hukubwa na tatizo la Upungufu wa damu. Kwa Tanzania zaidi ya nusu(57%) ya wajawazito wote wanakumbwa na tatizo la upungufu wa damu
Sababu za upungufu wa damu zipo nyingi zikihusisha; Uambukizo sugu au magonjwa sugu/chronic infection, Matatizo ya minyoo, Upungufu wa madini kama vile madini chuma/iron deficiency na upungufu wa vitamini muhimu kama vile vitaminB12 na vitamini B9/ Folate(folic acid) ambazo zina mchango mkubwa ktk utengenezaji wa damu mwilini
Hata hivyo upungufu wa damu huweza kusababisha matokeo hasi kwa Mama mjamzito na Mtoto aliye tumboni; Kwa mama hupatwa na matatizo kama maumivu ya kichwa, mikono na miguu kuwa ya baridi, Kizunguzungu, shida ya kupumua, Uchovu mkali na udhaifu wa mwili, kushindwa kutumia uwezo wake wa kiakili ipasavyo, kukosa hamu ya kula, kuyasikia mapigo ya moyo, ugonjwa wa moyo na hata kifo.
Kwa mtoto matokeo hasi ni kama; kushindwa kukua vizuri akiwa tumboni/intrauterine Fetal growth restriction, kuzaliwa kabla ya wakati/Njiti, kuzaliwa na uzito mdogo kupita kiasi, na mtoto kufia tumboni. Hata hivyo madhara ya baadae kwa mtoto kama vile Ukuaji usioridhisha/udumavu, maendeleo duni ya kiakili na kimwili, hatari ya kuumwa ugonjwa wa moyo, kuandamwa na tatizo la msongo wa mawazo, na uzito kupindukia huweza kutokea kwenye maisha ya mtoto aliyezaliwa na mama mwenye upungufu wa damu.
Ufanye nini/ nini kifanyike sasa kuepuka matatizo yote haya?
Save namba yangu hii hapa chini👇🏿 uweze kujipatia elimu hii na zingine bure kabisa baadae kupitia wsp status
Ukini save usisahau kunitumia jina lako na mimi niweze kuku save
“Let's connect for our future”