Wajue mapacha kumi maarufu zaidi duniani

Bitoz

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2015
Posts
30,823
Reaction score
126,553
Kuna aina mbili za mapacha ambazo ni mapacha walioungana na mapacha wa kawaida
Pia unaweza kusema mapema wanaofanana na mapacha wasiofanana
Sasa mimi nalenga kuwazungumzia mapacha wa kawaida ambao waliweza kufanya mambo mazuri au mabaya na kujipatia umaarufu mkubwa duniani

Kwa Afrika nadhani Okore Brothers a.k.a P Square ndio mapacha maarufu zaidi kutokana na shyghuli zao za kimuziki

...................... . ........... ..................................

10/Ronald"Ronnie" & Reginald"Reggie" Kray

Hawa mapacha waliishi maisha ya kijanjajanja tu kama ilivyo kwa viben ten vya mjini
Hawa umaarufu wao umetokana na tabia yao ya utapeli,wizi, mauaji,ukabaji na kila aina ya upuuzi waliokuwa wakiufanya katika kitongoji cha East End London mahali walipokuwa wakiishi miaka ya 1950 na 1960'
Pamoja na uhalifu wao huo waliofanya kwa kificho waliweza kumiliki klabu ya usiku na hivyo kifahamiana na mastaa kibao na hivyo kupata shavu kwenye vyombo vya habari na pia kupiga assist kwa mastaa
Mwaka 1968 walitiwa mbaroni na kutupwa jela maisha
Hawa Kulwa na Dotto waliutumia ufanano wao kama fursa ya kufayia uhalifu na hivyo kuwachanganya watu
 
Wakwanza kulike kuona na kucoment hii
 
9/Shawn & Aaron Ashmore

Walizaliwa Oktoba 7 mwaka 1979 nchini Canada wakiwa ni maoacha waliofanana kupitiliza
Wanapatikana zaidi kwenye kituo vha luninga cha ABC
Shawn alijipatia umaarufu kupitia X-men films wakati Aaron alionekana kwenye Warehouse 13

Kisha wote kwa pamoja wakacheza muvi matata ya Smallville ambapo watu walishindwa kung'amua kwamba ni watu wawili tofauti
 
8/Charlie & Craig Reid

Walizaliwa Machi 5 mwaka 1962
Hawa walikuwa na bendi yao waliyoiita The Proclaimersambayo waliianzisha mwaka 1983 wakiwa na miaka 19 tu tu

Walitikisa sana miaka ya 1980 na kibao chao cha I am Gonna Be {500 Miles}
 
7/Kin Narita & Gin Kanie

Hawa ni mapacha walioweka rekodi ya kuishi miaka mingi zaidi hapa duniani
Hawa ni raia wa Japan waliofariki mwaka 2000 mmoja akiwa na miaka 107 halafu mwingine akiwa katimiza miaka 108
Mwaka 1992 wakati wanaadhimisha miaka 100 walizindua album waliyoipa jina la Gin Chan & Kin Chan ambayo ilibamba vilivyo huko Japan kwa akina Takuma na kuuza nakala kibao
 
6/The Harp Twins

Sijajua tarehe yao wala mwaka wao wa kuzaliwa
Ni mapacha wa Kimarekani
Hawa ni wanadada mapacha warembo ambao umaarufu wao umeongezeka kutokana na video zao zilizojazana huko YouTube
Wametoa singo zaidi ya 80
 
5/James & Oliver Phelps

Walizaliwa Februari 25 mwaka 1986
Hawa ni mapacha maarufu huko kwa Malkia Elizabeth na dunianikwa ujumla
Hawa wanafahamika zaidi kama Wesley Brothers
Wanaonekana kwenye mfululizo wa filamu za Harry Porter
/b>
Katika filamu hizo huonekana wakiwa na nywele nyeusi au rangi zingine tofauti na uhalisia kutokana na kupaka rangi( ambapo kiuahilsia wana nywele za dark beown)
Kwwnye filamu za Harry Porter watu wengi wameshindwa kung'amua kwamba ni mapacha na sio mtu mmoja
 
4/Billy & Benny Loyd McCrary

Walizaliwa Disemba 7 1946
Hawa ni mapacha wanaoshikilia rekodi ya kuwa mapacha vibonge zaidi kuwahi kutokea duniani
Walikuwa na uzito wa jumla wa Paundi 1468 (Kg 670+)
Mmoja alifariki wakati wakiendesha pikipiki ya pamoja(pikipiki pacha) mwaka 1979.....walipendelea kuendesha pikipiki
Mwingine akafariki mwaka 2001 kwa ugonjwa
Makaburi yao yamejengwa kwa kuyaunganisha sehemu moja
 
3/Cameroon & Tayler Winklevoss

Walizaliwa Agosti 21 mwaka 1981
Hawa ni wataalamu wa kubuni na kutengeneza tovuti yaani wapo vizuri kwenye Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA/ICT)
Ndio waliomshawishi na kumvutia Mark Zuckerberg kuanzisha mtandao wa Facebook baada ya kumpa wazo
Pia wana kipaji cha kurusha mikuki na kuendesha mitumbwi na walishiriki pamoja katika michuano ya Olympic huko Beijing nchini China 2008
 
2/Ronde & Tiki Barber


Walizaliwa April 7 mwaka 1975 huko kwa Donald Trump au ukipenda sema ISA baby
Hawa ni wacheza mpira wa Marekani {American Football}
Ronde Barber anachezea Tampa Bay wakati Tiki anachezea New York Giants...
Wanafansna kama akina Rafael & Fabio Da Silva walipokuwa Manchester United na kuwachanganya makocha,marefa,wachezaji wenzao na mashabiki
Wakati wakichezea timu moja ilikuwa ni balaa kuwatofautisha
 
1/Ashley & Mary--Kate Olsen

Walizaliwa Juni 13 mwaka 1986 nchini Marekani
Hawa umaarufu wao inatokana na pesa walizonazo.....hawajafikisha hata miaka 35 lakini wana mkwanja mrefu wa kuweza kuwahonga hadi Sizonje na Bashite waamue kuuza nchi nzima ya Bongo na kutuacha wananchi tukipiga miayo
Wanatajwa kuwa wanawake matajiri # 10 duniani

Pia pengine ndo mapacha wenye mpunga mrefu zaidi duniani
Utajiri wao ni zaidi ya USD milioni 300
.
.
.
.
.
.
Mwisho
The Bitoz
................
 

Haha hawa mabonge mmh.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…