Wajue marais walioingia kwa kupindua Afrika

Ngosha Mashine

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2017
Posts
665
Reaction score
1,360
PAUL KAGAME WA RWANDA
Kagame alikulia mafichoni nchini Uganda , ambapo wazazi wake walikuwa wamemchukua akiwa mdogo wakati wa ghasia za watu wa kabila la Hutu na Tutsi ziliposambaa kabla ya taifa hilo kujipatia Uhuru wake kutoka kwa Ubelgiji.

Akiwa nchini Uganda alipata elimu yake katika chuo kikuu cha Makerere mjini kampala kabla ya kujiunga na vikosi vya Yoweri Museveni ambaye alikuwa amempindua rais Milton Obote mwaka 1986.

Kagame aliteuliwa kuwa afisa mkuu wa kitengo cha ujasusi na kupata sifa za ya mtu ambaye alikuwa hawezi kushawishika kiufisadi na kuweka sheria kali ya maadili.

Uongozi wa nchi unapobaki katika familia moja

Raia wengi wa Uganda walipinga uwepo wa rais huyo wa Rwanda nchini mwao , hatahivyo huku miaka ya 80 ikikaribia , Kagame na wanajeshi wakuu wa Rwanda waliotoroka taifa hilo walipanga uvamizi wa taifa lao.

Mwaka 1990 wakati ambapo kagame alikuwa akisoma katika kituo kikuu cha kijeshi huko Kansas Marekani , uvamizi huo ulioshirikisha Watutsi kutoka kwa jeshi la Uganda ulishindwa nguvu.

Katika vita hivyo wanachama watatu wakuu wa kundi la FPR waliuawa.

Kagame aliongoza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyositishwa Agosti 1993 na mkataba wa amani ulioahidi lakini haukugawa mamlaka kama ilivyohitajika

Mapema mwezi Aprili 1994 rais wa Rwanda Juvenal Habyarimana, Mhutu, aliuawa wakati ndege yake iliposhambuliwa na kuangushwa katika anga la mji wa Kigali .

Tukio hilo lilisababisha kampeni ya mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi kutoka kwa wenzao wa kabila la Wahutu .

Akijibu hilo Kagame , aliongoza jeshi la FPR lenye kati ya wanachama 10,000 hadi 14,000 dhidi ya vikosi vya Kihutu vilivyokuwa vikitekeleza mauaji hayo ya kimbari.

Akitekeleza mashambulizi ya moja kwa moja katika ngome za wapinzani , vikosi vya kagame vilifanikiwa kupunguza mauji hayo na kuchukua umiliki wa mji mkuu wa Kigali mapema mwezi Julai.

Kufikia wakati huo , hatahivyo , Zaidi ya watu 800,000 waliuawa katika mauaji hayo ya kimbari.

Wapiganaji wa FPR waliunda serikali mpya na rais wake akawa Pasteur Bizimungu, Mhutu , lakini nguvu za serikali hiyo zilionekana zikimilikiwa na Kagame ambaye akiwa na umri wa miaka 37 , alichukua wadhfa wa makamu wa rais na waziri wa ulinzi.

Mwaka 2000 alichaguliwa kuwa rais wa serikali ya mpito nchini Rwanda na bunge la taifa hilo. Tangu wakati huo amepigania urais na kushinda chaguzi zote.

RAIS SALVA KIIR WA SUDANI KUSINI
Tofauti Kagame, Kiir hakupindua serikali, bali aliongoza wanajeshi wake katika kunyakua uhuru wao na kuunda taifa jipya barani Afrika.

Kiir, alizaliwa katika ukoo wa Dinka kutoka jimbo la kusini la Sudan Kusini.

Wakati wa mzozo wa kwanza wa vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya 1955 hadi 1972, alijiunga na Anya Anya kundi la wapiganaji wanaotaka kujitenga kutoka kusini mwa taifa hilo katika vita dhidi ya serikali ilio na makao yake kaskazini mwa taifa hilo.

Baada ya vita kuisha aliingia katika jeshi la kitaifa la Sudan na mara moja akapatiwa wadhfa wa Luteni kanali. Wakati uadui uliporejea tena 1983, Kiir na wengine ikiwemo kanali John Garang de Mabior waliondoka katika jeshi la Sudan.

Akiwa pamoja na John Garang, Kiir alisaidia katika kubuni kundi la wapiganaji wa SPLM kabla ya kubadilika na kuwa Jeshi la raia wa Sudan la SPLA ambalo lilikuwa kundi la wapiganaji wa waasi wa Sudan Kusini likipigana dhidi ya seikali ya Sudan ilio na makao yake makuu kaskazini mwa taifa hilo.

Ndani ya SPLA. Kiir alikuwa mmoja ya makamu wakuu wa Garang na akachukua wadhfa wa naibu wa kamanda wa baraza la SPLA, pia alichukua wadhfa wa Ujasusi wa nyumbani pamoja na ule wa kigeni .

Wakati mgawanyiko ndani ya SPLM na SPLA ulipojitokeza 1990 na mapema 2000, Kiir alikuwa kiungo muhimu wa upatanishi na kusimamia tofauti zilizoibuka kati ya makundi yasiokubaliana.

Pia alikuwa mtu muhimu katika upatanishi na serikali ya kaskazini, ambayo ilisababisha makubaliano ya 2005 ambayo yalimaliza viata ya pili ya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan.

Kupitia masharti ya makubaliano hayo Jimbo la Sudan Kusini lilibuniwa 2005.

Julai 2005, Garang aliteuliwa kuwa rais wa jimbo hilo mbali na kuwa makamu wa rais wa kwanza wa taifa la Sudan.

Baada ya kifo chake ambacho hakikutarajiwa baadaye mwezi huo, Kiir alimrithi katika nyadhfa zote mbili.

Kifungu chengine cha makubaliano hayo ya CPA ni kwamba kulitarajiwa kufanyika kwa Kura ya maoni kubaini iwapo Sudan Kusini itakuwa nchi huru.

Raia wa Sudan Kusini walipiga kura mwezi Januari 2011 huku matokeo yakiunga mkono kauli ya eneo hilo kuwa taifa huru.

Baada ya kujitenga kwa Sudan Kusini tarehe 9 mwezi Julai 2011, Kiir alikuwa rais wa kwanza wa taifa la Sudan Kusini lililojipatia Uhuru.

RAIS YOWERI MUSEVENI WA UGANDA
Museveni alizaliwa na wazazi waliokuwa wafugaji wa ng'ombe na kwenda shule za wamishonari .

Akiwa anasomea shahada ya sayansi ya siasa na uchumi katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam Tanzania mwaka 1970, alikuwa mwenyekiti wa kundi la wanafunzi wa mrengo wa kushoto waliounga mkono mavuguvugu ya Kiafrika wakati huo.

Wakati Idi Amin alipochukua madaraka nchini Uganda mwaka 1971, Museveni alirudi nchini Tanzania mafichoni.

Akiwa nchini humo alianzisha kundi la Front for National salvation kundi lililomsaidia kumuondoa madarakani Amin 1979.

Museveni alishikilia nyadhfa kadhaa katika serikali za mpito na mwaka 1980 aliwania urais nchini humo.

Wakati Milton Obote aliposhinda uchaguzi ulioaminika kukumbwa na udanganyifu Museveni na rais wa zamani Yusufu Lule waliunda kundi la National Resistance Army NRM .

Museveni aliongoza kundi hilo lililo na wapiganaji waliojihami ambalo lilipigana vita vya msituni vya Gorilla dhidi ya utawala wa Obote.

Hatimaye NRM lilifanikiwa kumuondoa madarakani Obote mnamo tarehe 26 Januari 1986 ambapo Museveni alijitangaza kuwa rais wa taifa hilo.

Hadi wakati huo Museveni ameibuka mshindi katika chaguzi tofauti za urais wa hivi karibuni ukiwa ule wa 2021 ambapo alimshinda mpinzani wake Robert Kyagulani maarufu Bobi Wine.
 
Aboud Jumbe Mwinyi

Huyu aliingia Znz baada ya Mapinduzi ya 7th April,1972
 
Wapo wengi kama
Omar Al-bashir
Muammal Gaddaf
Robert Mugabe
Idriss Deby
Abdul Fatah Al-sis
Yahya Jameh
Idd Amin
Mobutu seseseko
Lawrent Kabila
John Okello
Charles Taylor
Meles Zenawi
Haile Mariam
Jerry Rawling
Blese Compaule
 
Wapo wengi kama
Omar Al-bashir
Muammal Gaddaf
Robert Mugabe
Idriss Deby
Abdul Fatah Al-sis
Yahya Jameh
Idd Amin
Mobutu seseseko
Lawrent Kabila
John Okello
Charles Taylor
Meles Zenawi
Haile Mariam
Jerry Rawling
Blese Compaule

also,Maaouya Ould Sid'Ahmed Taya wa Maurtania alipindua​

Wapo wengi kama
Omar Al-bashir
Muammal Gaddaf
Robert Mugabe
Idriss Deby
Abdul Fatah Al-sis
Yahya Jameh
Idd Amin
Mobutu seseseko
Lawrent Kabila
John Okello
Charles Taylor
Meles Zenawi
Haile Mariam
Jerry Rawling
Blese Compaule
Angeipata orodha hii Bila hata kuweka Nyama nyingi, uzi wake ungepata maana kubwa zaidi.
 
PAUL KAGAME WA RWANDA
Kagame alikulia mafichoni nchini Uganda , ambapo wazazi wake walikuwa wamemchukua akiwa mdogo wakati wa ghasia za watu wa kabila la Hutu na Tutsi ziliposambaa kabla ya taifa hilo kujipatia Uhuru wake kutoka kwa Ubelgiji.

Akiwa nchini Uganda alipata elimu yake katika chuo kikuu cha Makerere mjini kampala kabla ya kujiunga na vikosi vya Yoweri Museveni ambaye alikuwa amempindua rais Milton Obote mwaka 1986.

Kagame aliteuliwa kuwa afisa mkuu wa kitengo cha ujasusi na kupata sifa za ya mtu ambaye alikuwa hawezi kushawishika kiufisadi na kuweka sheria kali ya maadili.

Uongozi wa nchi unapobaki katika familia moja

Raia wengi wa Uganda walipinga uwepo wa rais huyo wa Rwanda nchini mwao , hatahivyo huku miaka ya 80 ikikaribia , Kagame na wanajeshi wakuu wa Rwanda waliotoroka taifa hilo walipanga uvamizi wa taifa lao.

Mwaka 1990 wakati ambapo kagame alikuwa akisoma katika kituo kikuu cha kijeshi huko Kansas Marekani , uvamizi huo ulioshirikisha Watutsi kutoka kwa jeshi la Uganda ulishindwa nguvu.

Katika vita hivyo wanachama watatu wakuu wa kundi la FPR waliuawa.

Kagame aliongoza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyositishwa Agosti 1993 na mkataba wa amani ulioahidi lakini haukugawa mamlaka kama ilivyohitajika

Mapema mwezi Aprili 1994 rais wa Rwanda Juvenal Habyarimana, Mhutu, aliuawa wakati ndege yake iliposhambuliwa na kuangushwa katika anga la mji wa Kigali .

Tukio hilo lilisababisha kampeni ya mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi kutoka kwa wenzao wa kabila la Wahutu .

Akijibu hilo Kagame , aliongoza jeshi la FPR lenye kati ya wanachama 10,000 hadi 14,000 dhidi ya vikosi vya Kihutu vilivyokuwa vikitekeleza mauaji hayo ya kimbari.

Akitekeleza mashambulizi ya moja kwa moja katika ngome za wapinzani , vikosi vya kagame vilifanikiwa kupunguza mauji hayo na kuchukua umiliki wa mji mkuu wa Kigali mapema mwezi Julai.

Kufikia wakati huo , hatahivyo , Zaidi ya watu 800,000 waliuawa katika mauaji hayo ya kimbari.

Wapiganaji wa FPR waliunda serikali mpya na rais wake akawa Pasteur Bizimungu, Mhutu , lakini nguvu za serikali hiyo zilionekana zikimilikiwa na Kagame ambaye akiwa na umri wa miaka 37 , alichukua wadhfa wa makamu wa rais na waziri wa ulinzi.

Mwaka 2000 alichaguliwa kuwa rais wa serikali ya mpito nchini Rwanda na bunge la taifa hilo. Tangu wakati huo amepigania urais na kushinda chaguzi zote.

RAIS SALVA KIIR WA SUDANI KUSINI
Tofauti Kagame, Kiir hakupindua serikali, bali aliongoza wanajeshi wake katika kunyakua uhuru wao na kuunda taifa jipya barani Afrika.

Kiir, alizaliwa katika ukoo wa Dinka kutoka jimbo la kusini la Sudan Kusini.

Wakati wa mzozo wa kwanza wa vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya 1955 hadi 1972, alijiunga na Anya Anya kundi la wapiganaji wanaotaka kujitenga kutoka kusini mwa taifa hilo katika vita dhidi ya serikali ilio na makao yake kaskazini mwa taifa hilo.

Baada ya vita kuisha aliingia katika jeshi la kitaifa la Sudan na mara moja akapatiwa wadhfa wa Luteni kanali. Wakati uadui uliporejea tena 1983, Kiir na wengine ikiwemo kanali John Garang de Mabior waliondoka katika jeshi la Sudan.

Akiwa pamoja na John Garang, Kiir alisaidia katika kubuni kundi la wapiganaji wa SPLM kabla ya kubadilika na kuwa Jeshi la raia wa Sudan la SPLA ambalo lilikuwa kundi la wapiganaji wa waasi wa Sudan Kusini likipigana dhidi ya seikali ya Sudan ilio na makao yake makuu kaskazini mwa taifa hilo.

Ndani ya SPLA. Kiir alikuwa mmoja ya makamu wakuu wa Garang na akachukua wadhfa wa naibu wa kamanda wa baraza la SPLA, pia alichukua wadhfa wa Ujasusi wa nyumbani pamoja na ule wa kigeni .

Wakati mgawanyiko ndani ya SPLM na SPLA ulipojitokeza 1990 na mapema 2000, Kiir alikuwa kiungo muhimu wa upatanishi na kusimamia tofauti zilizoibuka kati ya makundi yasiokubaliana.

Pia alikuwa mtu muhimu katika upatanishi na serikali ya kaskazini, ambayo ilisababisha makubaliano ya 2005 ambayo yalimaliza viata ya pili ya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan.

Kupitia masharti ya makubaliano hayo Jimbo la Sudan Kusini lilibuniwa 2005.

Julai 2005, Garang aliteuliwa kuwa rais wa jimbo hilo mbali na kuwa makamu wa rais wa kwanza wa taifa la Sudan.

Baada ya kifo chake ambacho hakikutarajiwa baadaye mwezi huo, Kiir alimrithi katika nyadhfa zote mbili.

Kifungu chengine cha makubaliano hayo ya CPA ni kwamba kulitarajiwa kufanyika kwa Kura ya maoni kubaini iwapo Sudan Kusini itakuwa nchi huru.

Raia wa Sudan Kusini walipiga kura mwezi Januari 2011 huku matokeo yakiunga mkono kauli ya eneo hilo kuwa taifa huru.

Baada ya kujitenga kwa Sudan Kusini tarehe 9 mwezi Julai 2011, Kiir alikuwa rais wa kwanza wa taifa la Sudan Kusini lililojipatia Uhuru.

RAIS YOWERI MUSEVENI WA UGANDA
Museveni alizaliwa na wazazi waliokuwa wafugaji wa ng'ombe na kwenda shule za wamishonari .

Akiwa anasomea shahada ya sayansi ya siasa na uchumi katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam Tanzania mwaka 1970, alikuwa mwenyekiti wa kundi la wanafunzi wa mrengo wa kushoto waliounga mkono mavuguvugu ya Kiafrika wakati huo.

Wakati Idi Amin alipochukua madaraka nchini Uganda mwaka 1971, Museveni alirudi nchini Tanzania mafichoni.

Akiwa nchini humo alianzisha kundi la Front for National salvation kundi lililomsaidia kumuondoa madarakani Amin 1979.

Museveni alishikilia nyadhfa kadhaa katika serikali za mpito na mwaka 1980 aliwania urais nchini humo.

Wakati Milton Obote aliposhinda uchaguzi ulioaminika kukumbwa na udanganyifu Museveni na rais wa zamani Yusufu Lule waliunda kundi la National Resistance Army NRM .

Museveni aliongoza kundi hilo lililo na wapiganaji waliojihami ambalo lilipigana vita vya msituni vya Gorilla dhidi ya utawala wa Obote.

Hatimaye NRM lilifanikiwa kumuondoa madarakani Obote mnamo tarehe 26 Januari 1986 ambapo Museveni alijitangaza kuwa rais wa taifa hilo.

Hadi wakati huo Museveni ameibuka mshindi katika chaguzi tofauti za urais wa hivi karibuni ukiwa ule wa 2021 ambapo alimshinda mpinzani wake Robert Kyagulani maarufu Bobi Wine.
General Tito Okelo umempangia kazi gani?
 
Back
Top Bottom