Wajue viumbe wa ajabu waishio angani

"ukweli ni
kwamba huchukuliwa na viumbe hao"

Ukweli huwa na uthibitisho naomba unithibitishie hilo hapo juu.
halafu mkuu ni bora ukabez kwenye suala zima la uthibitisho juu ya uwepo wa aliens hayo mengine yatakuja tuu...
 
Mkuu ishu ya Dinosaurs wanasayansi wanadai species hiyo imetoweka miaka million 60+ huko

Inakuwaje kupitia mifupa waweze kufahamu classifications ,namna wanavyozaliana,kula ,life style yao nk

Mifupa haiozi lkn zaidi ya miaka million60 hizo mifupa zibaki tu hvy hvy lzm zingeteketea na kuwa dust

Hii ishu ya dinosaurs ni kutupumbaza kama nadharia ya mtu wa kwanza alikuwa nyani

Zaidi ya million60+ Leo utambue classifications ,maisha ya mnyama huyu mpaka documentary wametengeneza

Sikubaliani na hao archeologies
 
MKUU wangu unaitaji kujisomea sana kupitia report za vyanzo vya kuaminika sio ku Google tu ukasoma ujui kaandika nani unakuja kufungua thread. kifupi uko juu juu sana kwenye mambo haya na utakua na busara kama usipoleta muendelezo wako Ila ukafanye research ili siku nyingine ufungue Uzi wenye mashiko. SHUKRANI
 
kwa namna hali ilivyo mashaka yamekuwa mengi siku hizi. mfn, kuna hii kitu imeibuka siku hizi ya masalia ya binadamu mwenye mwili mkubwa, ni kweli unaona wataalamu wa mambo ya kale wako busy kuchimba masalia. baadae utaona kweli picha nyingi tu za masalia ya mifupa ama fuvu ambalo pengine hata kwenye pickup haliingii, ila zimebaki hadithi tu! kwa wanao fatilia program moja mystery at the musium katika ch ya viasat history wamepata kuona baadhi ya vitu ambavyo watu waliwahi kuvichonga au kutengeneza na kisha kufukia ardhini kwa miaka kadhaa. kisha huvifukua na kutangaza wamechimbua masalia ya kale, badae huanza kutoza fedha kwa watakao taka kuona. walitengeneza pesa za kutosha, ila walio kuwa wanastukiwa wengi walitoroka ama kuhukumiwa vifungo.
mfn; kama mtakumbuka miaka ya karibuni kuna artist alitengeneza nguva kwa material maalum na kisha kumtupa pwani ya moja ya ufukwe (Ujerumani, 'sina hakika') nadhani wengi wanaikumbuka hii issue ilivyovuma kwenye mitandao, ila baadae jamaa alikuja kitoa clip namna alivyofanikisha zoezi lake.
hayo ni kwa yale tunayojua, je! ni mangapi tumefichwa?
safari bado ni ndefu ndugu, kama bado kuna wanao amini hata hili la allien dunia ya leo basi kazi ipo...
 
yaani unaenda mbele unarudi nyuma umesema wanaishi angani je mmewahi kuona wanapo ishi??????? pia umesema wana teknolojia kubwa kupita ya binadamu je mmeshawahi kuiona hiyo teknologia yao????????????????
kamammeshaona wanapoishi na hivyo vitu vingine leteni na uthibitisho sio maneno matupu tu..... hatudanganyiki😀😀😀😀
 
Ni mapepo tu
 
Umesema vyema lakini cha ajabu mtu kama wewe utakuta unaamini kwamba mungu yupo.!
 
Umesema vyema lakini cha ajabu mtu kama wewe utakuta unaamini kwamba mungu yupo.!
Ishu ya Mungu tofauti na dhana ya aliens nk

1.kuna uthibitisho nitakupa,duniani hakuna jambo la chance kila kitu kinatengenezwa mfano meli,gari,silaha,nyumba hazijatokea by chance bali zilitengenezwa na wanaadamu

Robot haikutokea by chance Bali mtu ndio aliyoitengeneza

Pia milima ,bahari,dunia,sayari, viumbe havijatokea by chance yupo aliyetengeneza na kuumba
So dhana nzima ya dini yeyote ile ni kuabudu basi huyo aliyetengeneza na kuumba hii dunia ndio anapaswa kushukuriwa

Jibu ya uthibitisho wangu Mungu ana exist sababu hakuna kitu kinachoitwa creation by chance..
 
Mystical stories, no credible source imeconfirm uwepo wa Ellien.
By the way according to space expertise definition ya ellien ni kitu chochote chenye uhai kilichopo nje ya dunia ( ambacho kijatoka duniani). Kiwe mmea,mnyama, bacteria nk...na co lazima kiwe na intelligence!!
 
Hakuna cha aliens wala nini. Huko ni kutufumba macho ili tusitafiti kwa yale yanayotokea, Hiyo ni mipango ya NASA
 
Alien ni jina la kiumbe wa kubuni, alibuniwa na watengeneza muvie, hakuna ili kunogesha muvie kwa kusimulia viumbe wa ajabu wasiowahi kuthibitika
 
Sasa wanaakili kuzidi binadamu inamaana huku juu kuna magari ya kisasa kuliko haya, na akili yao wanatumia kufanyia nn? Yasiwe ya akina Alpha holela au Abunuasi.
 
Umeanza kwa kuzunguka mno mkuu.. Go straight, to the point
 
Atakuuliza-huyo Mungu yeye kaumbwa/katengenezwa na nani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…