Elections 2010 Wajue wapinzani mahiri waliokaliwa kooni majimboni

Remmy siko juu hata kidogo ndugu yangu najaribu tu kutoa tathmini ya hali halisi kwa upande wa upinzani, kwani kuna post humu jf inaonyesha wa ccm walio kikaangoni majimboni

Ni ukweli ulioongea ktk post yako lakini ningependa kila mwana jf atoe tasmini na maoni yake kupitia jimbo alilopo ili kupata ukweli kuliko kuamini habari za kusikia. Mimi nipo kikazi jimbo la HAI kwa kimpindi cha wiki mbili sasa hapa HAI mjini mji wa BOMANG'OMBE MBOWE anawapeleka puta sana CCM asikuambie mtu kwa utafiti wangu mdogo usio rasmi nilioufanya FUYA KIMBITA mgombea wa CCM mbunge anayemaliza muda wake hali yake si nzuri kisiasa jimboni humu labda sikuzilizo baki kuelekea uchaguzi mambo yabadilike lakini mjini na vijijini mpaka sasa MBOWE amewashika CCM
 


Jamani tuwe wakweli na tujadili hoja kwa hoja na si kiushabiki. Naona Zitto anatajwa kuwa maji ya shingo jimboni kwake hivi kweli Zitto angekuwa anapelekwa mbio angeondoka jimboni na kwenda Jimbo la kibaha, mkoani lindi na sasa Bukombe kupiga kampeni. Embu tutafakari kwa umakini ungekuwa wewe ndio Zitto na jimboni mambo hayaendi vizuri ungeenda kuwapigia kampeni wagombea wa chama chako au ungebaki jimboni kupambana? embu vaa viatu vya Zitto halafu ujibu hii changamoto
 
PAULSS "usicheze mbali unga robo" OCT31
 
hii ndo demokrasia msiwe waoga! sisi wananchi tunataka kiongozi anayefaa mwisho wa siku chuma na chuma visuguane tupate kitu cha ukweli! CCM hawana jipya ukiona hao tu ndo wanaozungumziwa hamna anye wajali!
 

Kwa nini useme watagawana kura na kumwacha CCM anapeta? Mie nakwambia kuwa watachukua za CCM, hivyo mgombea wa CCM atapata kura kidogo na hao wapinzani ndo watakaoshindana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…