Wajue Watanzania na Serengeti Boys yao kabla ya Mashindano na baada ya Vipigo vya mfululizo

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Kabla ya Vipigo vya Nigeria na Uganda maoni yao yalikuwa haya……

Serikali kupitia Wizara na Waziri Mwakyembe
“ Hii ndiyo Timu inayoenda Kututoa Kimasomaso Watanzania na hili Kombe tutalibeba hapa hapa Dar es Salaam linapofanyika “

TFF kupitia Rais wake Karia
“ Kama kuna Timu ya Taifa ya Tanzania ambayo inanipa raha na amani ni hii ya Serengeti Boys kwani wameiva kabisa, tumewaweka Kambi nchi mbalimbali na wameshinda Vikombe vingi mno na huu Ubingwa tunauchukua na Brazil tunaenda iwe isiwe “

Kocha Mkuu Milambo
“ Njooni Uwanjani muone jinsi Watoto ( Serengeti Boys ) wanavyocheza mpira kama wa Barcelona na Liverpool FC na kuwapeni raha Watanzania kwani kama kuna mwaka ambao Tanzania tuna Timu bora ya Vijana basi ni huu wa 2019 na hii Timu “

Mlezi Mzee Mengi
“ Wajukuu zangu naamini hamtaniangusha na kama mkiitumia ile ile Falsafa yangu ya I can I must and I will Brazil mnaenda na najua katika hizi Timu zote hakuna hata moja ya Kuwatisheni na nina uhakika hili Kombe mnalibeba “

Waandishi wa Habari wa Tanzania
“ Kwa Maandalizi ya Serengeti Boys hii hata wakitupeleka Kombe la Dunia Kombe tunalibeba kwani Timu ina Wachezaji wazuri, wenye Maumbile mazuri na wote wana Vipaji vikubwa tena vya kuzidi akina Messi na Ronaldo hivyo hawa CAF watukabidhi tu Kombe letu hili “

Watanzania
“ Huu ni mwaka Wetu kwani Nyota njema ilianza kwa Simba SC, Bondia Mwakinyo na Taifa Stars hivyo hata hawa Vijana Wetu Serengeti Boys tuna uhakika watafanya makubwa zaidi ya hao na bado sijaona Timu ya nchi yoyote kati ya hizi zilizokuja zinaweza Kucheza na Serengeti Boys hii iliyoiva na kusheheni Vipaji vingi “

Baada ya Vipigo viwili vya mfululizo vya Nigeria na Uganda maoni yao yakageuka ghafla na kuwa hivi…

Serikali kupitia Wizara na Waziri Mwakyembe
“ Wameponea tu chupuchupu ila hata hivyo wameshatutambua kuwa Tanzania si ya mchezo mchezo “

TFF kupitia Rais wake Karia
“ Bahati tu haikuwa upande Wetu ila huko mbele katika Michuano ijayo tuna uhakika wa Kubeba hili Kombe “

Kocha Mkuu Milambo
“ Pamoja na Kufungwa michezo miwili hii na Nigeria na Uganda bado Tanzania kupitia Serengeti Boys tuna nafasi ya Kufuzu Kibahati kwani hata Bahati nayo ni sehemu ya Mchezo katika Soka kwahiyo Watanzania msife Moyo nafasi bado ipo tena Kubwa sana tu n Brazil tunaenda “

Mlezi Mzee Mengi
“ Na laana yangu iwapateni nyie Vijana wote kwani mmeniangusha kabisa japo Kimoyomoyo nimefurahi kuwa Hela zangu zimeponyeka na Magari yamepona hivyo mtaendelea Kupanda DalaDala hadi mkome na Siku zingine mjifunze na msifungwe fungwe hovyo “

Waandishi wa Habari wa Tanzania
“ Nigeria na Uganda wamecheza Vijeba wengi sana, tumeonewa na TFF wasikubali wakakate Rufaa CAF kwani bado hawajachelewa “

Watanzania
“ Kipa mbovu, mabeki wabovu na Kocha hafai kabisa na Tanzania labda lije Kombe la Kufanya Ngono tu ndiyo tunaweza Kulibeba kila mwaka ila kwa Mpira wa Miguu nadhani tumeshalaanika nao “

Tupo pamoja.
 
Mwalim wangu aliwahi kuniambia kuwa watu wanajua kila kitu, akasema ukifaulu watasema tulijua tu unafaulu maana una tabia nzuri, huna maringo, unajituma.

Hao hao siku ukifeli watasema tulijua tu lazima ufeli maana hujitumi, unajiona sana.

Kwa hiyo saa ingine binadamu ni kama bendera hufuata upepo.
 
Kama litakuja tokea Pambano la kubishana kuhusu soka iseeee watanzania tutachukua kombe

Afu sijajua kwann watanzania tunapenda unafki
 
Kama litakuja tokea Pambano la kubishana kuhusu soka iseeee watanzania tutachukua kombe

Afu sijajua kwann watanzania tunapenda unafki
 
Kama litakuja tokea Pambano la kubishana kuhusu soka iseeee watanzania tutachukua kombe

Afu sijajua kwann watanzania tunapenda unafki
 
[emoji16][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji16][emoji16] igweeeeeee
 
Mm nipo against sana na kuwaahidi watoto mamilioni hao bado wadogo sana wanaenjoy kucheza mpira waacheni wacheze mpira mnawachanganya na mihela hiyo
r
 
Si walikuwa wanasifiwa kwa nidhamu ya hali ya juu . huyo nidhamu haijawapa mafanikio??
 
Mm nipo against sana na kuwaahidi watoto mamilioni hao bado wadogo sana wanaenjoy kucheza mpira waacheni wacheze mpira mnawachanganya na mihela hiyo
r

Na ( technically ) Kosa kubwa hadi kupelekea kupata hayo matokeo ya aibu lilianzia hapo katika hizo ahadi. Tumeaibika na Kujiaibisha mno Tanzania na hasa kama Waandaaji wa hii Michuano.
 
Kocha osca nasema sukuma ndani. Walesi karia weka ndani. Bsshite sukuma ndani mzee wa mil 20 weka ndani. Mmetuabisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…