Wajue Wazelote, magaidi wa Kiisraeli waliotamalaki enzi zile za Yesu, husemekana kuwa ndio kundi la kwanza la magaidi duniani

Raphael Mtui

Member
Joined
Nov 26, 2024
Posts
78
Reaction score
204
Kaskazini mwa nchi ya Israeli, kwenye miteremko ya milima ya Golani, (Golan Heights) ndani ya kijiji kiitwacho Gamala, katika jimbo la Galilaya, alizaliwa kijana mmoja aliyepewa jina la Yuda.

Kijana Yuda alikuja kuwa mtu msumbufu nzima ya Israeli! Kipindi hicho Waisraeli walikuwa wakipitia shubiri ya kutawaliwa na Warumi, ingawa hawakuonesha 'nyongo' alizozionesha kijana huyu.

Pamoja na kuzaliwa jimboni Galilaya, inaonekana katika ujana wake alisafiri kwenda Yerusalemu jimbo la Yudea, pengine katika harakati za kwenda 'kutafuta maisha.'

Alipofika kule, alikutana na mchakato mzima wa jimbo la Yudea kutangazwa rasmi kuwa milki ya serikali ya Rumi.

Kijana Yuda hakuwa na 'simile' akajitosa kuanza vuguvugu ambalo lilikuja kuzaa kundi hatari la kigaidi lililoitwa Wazelote. Kila aliposimama, alihubiri kwa Wayahudi wenzake kwamba ni dhambi isiyo na mfano kukubali kutawaliwa ama kuwa koloni la nchi nyingine tena ya kipagani kama Rumi.

Kama tujuavyo, hakuna mtu asiyepata wafuasi duniani hata awe anahubiria watu wale majani! Yuda alipata wafuasi wengi, na mara kukazaliwa vuguvugu la watu wenye hasira, 'wasioelewa somo, wasio na dogo', wanachojua ni kwamba wakiona mtu mwenye asili ya Rumi au Myahudi mwenye urafiki na Warumi, basi 'wanakula' roho yake!

Ingawa Yuda hakuishi miaka mingi, lakini nyuma aliacha mawazo kwenye mioyo ya baadhi ya Wayahudi ambao waliendelea kuisumbua serikali ya Rumi, na hatimaye kule mwishoni kusababisha Warumi wawapige kwa pigo kuu lililodumu kwa miaka karibu elfu mbili kwa taifa zima la Israeli.

Tutaeleza kwa undani hapo mbeleni. Biblia imemtaja kijana Yuda wakati yule Mzee Gamalieli alipowasihi wenzake katika baraza la Wayahudi wasihangaike kuwazuia kina Mtume Petro kumhubiri Yesu kwani kama hawakutoka kwa Mungu wataishia kupotea tu kama kijana Yuda wa Galilaya.

Matendo 5:37
Baada ya mtu huyo aliondoka Yuda Mgalilaya, siku zile za kuandikwa orodha, akawavuta watu kadha wakadha nyuma yake, naye pia akapotea na wote waliomsadiki wakatawanyika.

Kama utakuwa unajiuliza kuhusu Theuda aliyetajwa kwenye Matendo 5:36, huyo hakuwa chochote zaidi ya mchawi mmoja aliyejipatia umaarufu kidogo na kuishia kuuawa siku alipowapeleka wafuasi wake mto Yordani na kusema anataka kuyagawanya maji ya Mto Yordan kama ambavyo Nabii Yoshua alivyofanya. (Soma Yoshua sura yote ya tatu).

Aliishia kuvamiwa na askari na kuuawa pamoja na baadhi ya wafuasi wake.

Turudi kwa Yuda Mgalilaya:

Hasira za kijana Yuda ziliwaka zaidi pale ambapo serikali ya Rumi ilitoa tangazo la kufanyika sensa kwa watu ili watozwe kodi kisawasawa.

Wote tunakumbuka ile sensa ama orodha iliyoandikwa kwenye kitabu cha Luka, sensa ambayo ilisababisha Yusufu na Mariamu wasafiri kutoka Galaliya kwenda Bethlehemu ambako mtoto Yesu alienda kuzaliwa.

Luka 2:1-2.
Siku zile amri ilitoka kwa Kaisari Augusto ya kwamba iandikwe orodha ya majina ya watu wote wa ulimwengu.

Orodha hii ndiyo ya kwanza iliyoandikwa hapo Kirenio alipokuwa liwali wa Shamu.

Yuda alikuja juu akipinga wazi wazi sensa hii, na kusisitiza Wayahudi wasikubali kujiorodhesha na kamwe wasikubali kulipa kodi.

Alikuwa akiwaonya vikali Wayahudi kwamba kulipa kodi kwa Kaisari kulikuwa ni uasi mkubwa kwa Mungu wao kwani wanatoa fedha kwa ajili ya kwenda kujenga ufalme wa kipagani.

Ukweli ni kwamba Yuda alikamatwa na kuuawa akiwa bado 'mbichi' kabisa. Ile kanuni ya mtoto wa nyoka ni nyoka ilijitokeza hapa, kwani Yuda alikuwa amezaa watoto wenye ghadhabu za kiharakati kama zake.

Baada ya baba yao kuuawa, watoto wawili waitwao Simoni na James waliendeleza harakati za baba yao, hadi walipokuja kukamatwa na kuuawa baadaye sana kwa kutundikwa msalabani wakiwa wazee.

Sasa twende hivi:

Moja ya vitu ambavyo Yesu alivifanya vikawashangaza watu hadi leo, ni pamoja na kitendo chake cha kumchagua Simoni Mzelote kuwa moja ya wale Mitume wake kumi na wawili. (Luka 6:15)

Ukweli ni kwamba, hata leo huenda tukamshangaa pale tu tutakapowajua Wazelote hasa walikuwa ni watu wa namna gani.

Lakini bado tutarudi pale pale kwamba, Mungu wetu tunayemwabudu kupitia Kristo, anazidi kuuhakikishia ulimwengu kwamba ANA UWEZO WA KUMZAA MTU MARA YA PILI, MTU HUYO AKABADILIKA NA KUWA KIUMBE KIPYA, HAIJALISHI ALIKUWA MTU MBAYA NA MWOVU KIASI GANI.

Ndio hapa tusingetegemea mtu wa kaliba ya mauaji kama Mtume Paulo kuwa Mkristo namba moja katika historia nzima ya Ukristo, akiwazidi hata wale mitume kumi na mbili walioishi na Kristo muda wote.

Stori ya WAZELOTE iko hivi:

Wakati Bwana Yesu akiwa bado kijana mdogo, mnamo mwaka 6AD, tayari mawazo ya Yuda Mgalilaya yalikuwa yameshapandwa kwenye mioyo ya vijana kadhaa wa Kiyahudi.

Mawazo haya yalikuja kuzaa kundi hatari lililoitwa Zealots, ama kwa Kiswahili tunawaita Wazelote. Kwa vitendo walivyovionesha kwa ulimwengu, wamekuja kuwa na 'heshima' ya kuwa magaidi wa kwanza duniani.

Zealots walikuwa kundi tishio kweli kweli, lenye kuogopeka kwa vitendo vyao vya mauaji, mabavu, fujo, kuchoma nyumba na mali za watu.

Kutokana na staili waliyotumia ya kutekeleza ukatili na mauaji, jamii ilizoea kuwaita kwa kutumia neno la Kigiriki la 'Sicarii' kwa Kiswahili 'Wazee wa visu'.

Walikuwa wakibeba visu vya makali kuwili au sime na kuzificha kwenye nguo zao, na walipogundua wamempata mlengwa wao, walikuwa wakimvizia na kumshambulia kwa kumchoma visu kutokea nyuma mgongoni.

Iko hivi, neno 'zeal' ni neno la kawaida linalomaanisha hamu au kiu kubwa na utayari mkubwa wa kuhakikisha lengo fulani linatimia hata kama ni kwa gharama kubwa kiasi gani.

Si dhambi mtu kuwa na hiyo 'zeal' kama akiitumia sawasawa na Neno la Mungu.

Tujiulize tena swali hili muhimu: HAWA WAZELOTE WALIKUWA WANATAKA NINI? KWA NINI WALIKUWA WANAFANYA UKATILI HUU? NA JE, WALENGWA WAO HASA WALIKUWA KINA NANI?

Kimsingi, Wazelote au Uzelote (Zealotism) kilikuwa ni chama cha siasa nchini Israeli, lakini mwandishi maarufu wa historia za Israeli Josephus anaongeza kwa kuwaita Wazelote kama dhehebu la nne la dini ya Uyahudi baada ya Mafarisayo, Masadukayo, Essenes na sasa hawa Wazelote.

Chama hiki au dhehebu hili lilianzishwa kwa lengo kuu la kupingana na serikali ya utawala wa Rumi (Roman Empire) ambayo ilikuwa ikitawala Israeli kwa wakati huo.

Yaani, kila pumzi waliyovuta, kila hatua waliyopiga, kila pigo la mioyo yao, na kila walichofanya kiliakisi ajenda moja tu, kuuondoa utawala wa Warumi katika nchi yao.

Tukumbuke kuwa, nchi ya Yuda na jiji la Yerusalemu ilitangazwa rasmi kuwa jimbo la serikali ya Rumi mwaka 6AD.

Kitendo hiki kilizaa Wayahudi wenye hasira kali walioungana na kuanzisha vuguvugu la kupinga utawala huo, wakifuata mawazo ya Yuda kama 'Kinjekitile' wao.

Walisisitiza kwamba Israeli kama nchi takatifu haitakiwi kutawaliwa, tena na wapagani.

Walipinga dini za kipagani za Warumi, wakapinga vikali wananchi kutozwa kodi na serikali ya kigeni ya Rumi.

Walikataa matumizi ya sarafu za kirumi zenye picha ya Mfalme wa Rumi aliyekuwa mungu wa Warumi. Kwa wakati ule, Wayahudi walioteuliwa kufanya kazi ya kukusanya kodi walionekana ni wasaliti, na watenda dhambi wakubwa, yaani ukusanyaji kodi ulionekana ni dhambi kama dhambi zingine.

Tunajua neno 'watoza ushuru' lilivyo na picha mbaya katika Agano Jipya.

Watoza ushuru pia walikuwa wakishambuliwa na kuuawa na Wazelote.

Ingawa Wazelote walikuwa watu wa dhehebu la kidini kabisa, na tena walikuwa na mifanano mingi na dhehebu pendwa la Mafarisayo, lakini waligubikwa na vitendo vya kibabe, unyang'anyi, fujo, mabavu, mauaji, na walengwa wao walikuwa ni watu wenye asili ya Rumi, maafisa wa serikali ya Rumi, na wanajeshi wa Rumi.

Lakini pia, hata Wayahudi wenzao ambao walionesha kuridhia kutawaliwa na serikali ya Rumi nao 'waliona cha mtema kuni'.

Pia, Wazelote walipogundua kuna Myahudi ana urafiki au ukaribu na Warumi au mtu mwenye asili ya Kirumi, naye aliuawa, nyumba yake kuteketezwa, na hata mali zake kuchukuliwa kimabavu.

Kwa kifupi kabisa tuseme hivi, Wazelote walikuwa tayari kufanya kitu chochote mradi tu Warumi waondoke wawaachie nchi yao. Hawakujali wala kuogopa.

Hawakuonesha dalili ya huruma au ya hofu. Ndio maana ulimwengu wa leo umewaita ni moja ya Magaidi wa kwanza kutokea hapa duniani.

Yule Baraba aliyekuwa mashuhuri (Mathayo 27:16) na kufungwa kwa sababu ya mauaji na fitina jijini Yerusalemu, (Marko 15:7) alikuwa Mzelote. Vitendo vyake na dhamira aliyokuwa nayo ilifanania na Wazelote.

Wazelote waliendelea na harakati zao kwa muda mrefu, na kundi lao lilikua na kuongezeka.

Yesu alipoanza kuwa maarufu, Wazelote walitegemea atatumia ushawishi wake kuwaunganisha Wayahudi kwa pamoja ili waufurushe utawala wa Kirumi.

Lakini baada ya kuona Yesu hahangaiki kupingana na Warumi, na waliposikia anasema '..ya Kaisari mpe Kaisari,..' (Marko 12:17) hawakufurahia kabisa!

Walidhani Yesu ni mwanamapinduzi na mwanaharakati aliyekuja kuwataka watu wabebe silaha kuwashambulia Warumi.

Hawakujua Yesu alikuja kwa 'mission' kubwa kuliko hiyo. Yesu alikuja kuangusha ngome nzito zaidi kuliko Rumi, yaani kuvunja nguvu za dhambi katika maisha ya mwanadamu, kuleta uhuru wa milele, naam uzima wa milele kwa ulimwengu mzima.

Biblia haijawahi kuwazungumzia Wazelote, wala hatuna rekodi ya mahali Yesu akiwataja.

Mwaka 66AD, Wazelote walianza vita kubwa na vurugu kubwa kiasi kwamba walipata ushindi dhidi ya serikali ya Rumi! Lakini kufurushwa kwa Warumi kulisababisha balaa la milenia! Ndio! Milenia mbili nzima! Miaka elfu mbili ya msoto!

Serikali nzima ya Rumi iligundua kuwa Wazelote sio vijana wa 'kuchukulia poa.' Mwaka 70AD, Mfalme wa Roman Empire alituma jeshi kubwa kwenda kuvamia jiji la Yerusalemu, ambapo jiji zima la Yerusalemu lilibomolewa na kuteketezwa, na sio hivyo tu, Hekalu la Yerusalemu lilibomolewa na kuteketezwa kabisa.

Wazelote 73 waliokuwa wamejificha kule Masada walipogundua wanakaribia kukamatwa na majeshi ya Rumi, waliamua kujiua kabla hawajakamatwa!

Wayahudi walipojaribu tena kufanya uasi kwa uongozi wa Bar Kokhiba, ndipo hatimaye Mfalme Hadrian wa Roman Empire alipotangaza marufuku ya Wayahudi ambao ni wenyeji kuishi jijini kwao Yerusalemu.

Wayahudi wote walifukuzwa nchini kwao!Si hivyo tu, hata jina la jiji la Yerusalemu likafutwa, likaitwa Aelia Capitolina, na Israeli nzima ikaitwa Palestina, na kuanzia hapo nchi ya Israeli ikafutwa kabisa katika ramani ya dunia!Dunia ilikaa bila kuwa na nchi ya Israeli kwa karibu miaka 2000 hadi mwaka 1948 Israeli ilivyoundwa upya na kujitangaza kama taifa na nchi katika ramani ya dunia.

Tuseme hivi, Wazelote walichangia kwa sehemu kubwa kusababisha unabii wa kuharibiwa kwa jiji la Jerusalem na Hekalu kama manabii walivyotabiri akiwemo Yesu aliyekazia kwamba Hekalu litabomolewa kiasi ambacho hakuna jiwe litakalosalia juu ya jiwe. (Mathayo 24:2, Marko 13:2 na Luka 21:6).

Hii ni moja ya Topics zilizomo kwenye kitabu chetu kiitwacho IJUE ISRAELI.

Katika kitabu hicho, waandishi wamejikita kujibu swali linaoulizwa mara kwa mara la Israeli inatuhusu nini sisi Wakristo? Kuna ulazima gani wa sisi kujifunza na kuifuatilia Israeli? Na je, Israeli kuwa taifa teule ina maana uteule wao unatokana na wao kuwa watu wema wanaompendeza Mungu?

Katika kitabu hiki, wamekuwekea ile miujiza mikubwa mitano ya kivituko iliyotokea hekaluni kuwaashiria Wayahudi wanakosea kwa kuweka imani kwa hekalu badala ya kwa Yesu. Usiache kujua mambo ya ajabu yaliyotokea hekaluni na baada ya Yesu kusulibiwa na kuleta fadhaa kubwa kwa Wayahudi wakati ule kabla hekalu halijabomolewa na Warumi mwaka 70AD.

Pia, waandishi wamekuonesha mahesabu kamili ya unabii wa Ezekiel jinsi alivvyotabiri Israeli itapata uhuru mwaka 1948, na tukaeleza kwa upana ile stori ya kusisimua ya jinsi mambo yalivyoenda ile tarehe 14 May walivyopata uhuru. Lile tamko rasmi la uhuru wa Israeli hatimaye limetafsiriwa kwa Kiswahili, na kuwekwa ndani ya kitabu hiki.

Hali kadhalika wamekupa stori yote ya maajabu jinsi Israeli ilivyofutwa kwenye ramani ya dunia kwa miaka karibu 2000 na bado ikazaliwa tena, na tena kuwa simba tishio. Tumeorodhesha vita vyote walivyopigana tangu wapate uhuru na bado wakashinda kwa kishindo licha ya kushambuliwa na muungano wa majeshi makubwa.

Katika kitabu hiki utapata historia nzima ya taifa la Israeli tangu pale kwenye tukio la kitabu cha Mwanzo 12 Ibrahimu alipoitwa, historia hiyo ikaja hadi mwaka 2024. Historia hii ya kusisimua sio ya kukosa kabisa, kwa kuwa matukio yote muhimu yaliyotokea kwa Israeli yameorodheshwa.

Pia, utapata kwa undani historia tukufu ya Hekalu la Yerusalemu, hekalu la kwanza lililobomolewa na Nebukadreza na la pili lililokuja kubomolewa na Warumi mwaka 70AD.
Kitabu kimeangazia kwa nini Wayahudi hawajafanikiwa kujenga hekalu lingine mpaka leo, vikwazo vya ajabu walivyokutana navyo wakati wanajaribu kujenga hekalu la tatu ikiwemo moto uliokuwa unatokea ardhini na kuwachoma wajenzi kiasi cha kufanya ujenzi usimame. Pia, tumeeleza kwa undani juu ya michakato yote iliyofanywa na Waisraeli ya kupata ng'ombe mke mwekundu asiye na kipaku ambayo imefanyika dunia nzima pasipo mafanikio.

Pia utapata kujua kiundani namna ya kutofautisha Wasamaria na Wayahudi. Fahamu chanzo cha Wasamaria, na walikopotelea na upate kujua vizuri makundi hayo.

Kitabu hiki kina kurasa 142, kwa shilingi 15,000 unakipata kama soft copy.

Wasiliana nami kwa namba 0762731869, piga au whatsapp.

Raphael Mtui.
 
Chanzo gani kina history ya hao wazelote
 
Promo as usual
 
Back
Top Bottom