Wajukuu wa Ibrahimu katika picha, Kuhani na Mwalimu Musa Richard Mwacha na Sheikh Mkuu Mufti Abubakar Zubeir

Wajukuu wa Ibrahimu katika picha, Kuhani na Mwalimu Musa Richard Mwacha na Sheikh Mkuu Mufti Abubakar Zubeir

mama D

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2010
Posts
19,981
Reaction score
35,581
Upendo + Umoja + Mshikamano = Amani

IMG-20230603-WA0008.jpg



MWANZO 17: 1-22

"Abramu akaanguka kifudifudi. Mungu akamwambia, akasema, Mimi, agano langu nimefanya nawe, nawe utakuwa baba wa mataifa mengi.

Agano langu nitalifanya imara kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, na vizazi vyao, kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako.
Nami nitakupa wewe na uzao wako baada yako nchi hii unayoikaa ugeni, nchi yote ya Kanaani, kuwa milki ya milele; nami nitakuwa Mungu wao.
Mungu akamwambia Ibrahimu, Nawe ulishike agano langu, wewe na uzao wako kwa vizazi vyao baada yako.
Hili ndilo agano langu utakalolishika, kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, Kila mwanamume wa kwenu atatahiriwa.

Mungu akamwambia Ibrahimu, Sarai mkeo, hutamwita jina lake Sarai, kwa kuwa jina lake litakuwa Sara. Nami nitambariki, na tena nitakupa mwana kwake, naam, nitambariki, naye atakuwa mama wa mataifa, na wafalme wa kabila za watu watatoka kwake.

Ibrahimu akamwambia Mungu, Lau kwamba Ishmaeli angeishi mbele yako.

Mungu akasema, Sivyo, lakini Sara mkeo atakuzalia mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake Isaka. Nami nitafanya agano langu imara kwake kuwa agano la milele kwa ajili ya uzao wake baada yake.

Na kwa habari za Ishmaeli nimekusikia, nimembariki, nitamzidisha, nami nitamwongeza sana sana. Atazaa maseyidi kumi na wawili, nami nitamfanya awe taifa kuu.

Bali agano langu nitalifanya imara kwa Isaka, ambaye Sara atakuzalia majira kama haya mwaka ujao. Mungu akaacha kusema naye, akapanda kutoka kwa Ibrahimu."


Mungu ibariki Tanzania
 
Bali agano langu nitalifanya imara kwa Isaka, ambaye Sara atakuzalia majira kama haya mwaka ujao. Mungu akaacha kusema naye, akapanda kutoka kwa Ibrahimu."
Ujukuu wao kwa Ibrahim unakujaje ilhali wao ni wa Bantu?
 
Back
Top Bottom