wajumbe hawa wanatakiwa wapewe pongezi

uswaa

Member
Joined
Mar 4, 2014
Posts
55
Reaction score
20
PANDU, MAHALU LISU SIMBACHAWENE MDEE MWL OLOCHU UMMY MWALIMU MNYIKA OLESENDEKA VICENT MBOWE MACHALIII LIPUMBA wengine tuwataje mtzamo wangu wengi hawajali wako kimaslahi zaidi ilimradi kiingie mfn kipindi cha posho wote wanafungua midomo naamini wengi ukiwaulizw juu ya rasimu hawajui kitu hawasomi kinachoendelea
 
. Tangu kuanza kwa Bunge Maalumu la
Katiba, Februari 18 mwaka huu, wajumbe watano
wanaonekana kuwa ndio wachangiaji wakuu
katika mjadala wa Rasimu ya Kanuni za Bunge
hilo.
Bunge hilo la Katiba limekuwa likijadili Rasimu ya
kanuni za Bunge kwa takriban wiki moja sasa na
mjadala huo bado hilo haujamalizika kutokana na
mivutano miongoni mwa wajumbe kuhusu baadhi
ya vifungu vya kanuni hizo.
Pamoja na Bunge hilo kuwa na wajumbe 629,
wanaochangia kila mara ni Mbunge wa Simanjiro
(CCM), Christopher Ole Sendeka, Mbunge wa
Kigoma Mjini (CCM), Peter Serukamba, Mbunge
wa Nzega (CCM), Hamisi Kigangwalla, Mbunge wa
Ubungo (Chadema), John Mnyika (Chadema) na
Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania
(CWT), Ezekiel Oluoch.
Mbali na kuchangia, wakati mwingine wajumbe
hao wamekuwa wakinyoosha mikono au
kusimama kwa lengo la kuchangia, lakini
wanakosa nafasi.
Mfano mzuri ilikuwa ni jana wakati wa mjadala
kuhusu Rasimu ya Kanuni za Bunge hilo, wakati
Ole Sendeka na Oluoch waliposimama na
kuchangia.
Katika mjadala wa juzi, wajumbe hao wawili kila
mmoja alichangia mara tatu na mara nyingi
walipochangia hoja zao ziliungwa mkono na
wajumbe wengi.
Kigwangalla naye hayuko nyuma kwani katika
mjadala wa juzi alipewa nafasi mara mbili
kuchangia na wiki iliyopita huchangia mara mbili
kwa siku isipokuwa siku moja tu ambayo
alichangia mara moja.
Mjumbe mwingine ni Mnyika ambaye katika
mjadala wa juzi alichangia mara mbili kuhusu
mkanganyiko juu ya kuchagua aina ya ugaji wa
kura.
Naye Serukamba amekuwa mchangiaji wa karibu
kila siku na Ijumaa iliyopita alichangia kuhusu
kifungu cha 37 na 38 cha Rasimu ya Kanuni
hizo.
Sasa imekuwa jambo la kawaida kwa wajumbe
hao kuchangia katika Bunge hilo.
 

Wakuu tuchangie kwa vyeo halisi vya wajumbe. Oluoch ni naibu katibu mkuu wa CWT. Katibu mkuu ni Yahya Msulwa aliyekuwa mjumbe wa tume ya warioba.
 
Nitampongeza mbunge yeyote atakayeomba muungano uvunjike, awe katoka bara au visiwani, wacha uvunjike watu waelee kwenye maji ndio wawe na heshima
 
Nitampongeza mbunge yeyote atakayeomba muungano uvunjike, awe katoka bara au visiwani, wacha uvunjike watu waelee kwenye maji ndio wawe na heshima

hatupi tayari kupoteza muungano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…