Wajumbe hawana makosa, ni makosa ya waliowapa madaraka

Wajumbe hawana makosa, ni makosa ya waliowapa madaraka

Zygot

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2016
Posts
2,265
Reaction score
2,919
Kuna lawama nyingi kwa wajumbe juu ya maamuzi yao. Binafsi nawasamehe. Angalia nafasi wanazopewa kwa miaka mitano; Bila mshahara, bila ofisi, ghafla paa! Katibu anatangaza eti watia niya watapigiwa kura na wajumbe. Hao watia niya, mmojawapo ni mbunge aliyepewa mshiko wa milioni 250. Kwa miaka mitano iliyopita hakuwahi kuwatembelea. Mjumbe afanye nini zaidi ya kuomba kugawana manufaa ya nafasi hiyo?

Tatizo ni yule aliyewapa madaraka ya kuchuja wagombea. Alitegemea mtu asiyelipwa mshahara asimamie haki na ubora anaoutaka? Siyo Duniani.

Sasa tujiandae na aina ya viongozi waliotokana na wajumbe hao. Bahati mbaya hata rais ajaye anategemea, wamempa wanaofaa. Ninachohisi yeye tayari analo baraza la mawaziri kwa wachache bora na wale atakaowateua. Wengine bungeni wataendelea na vituko vya kusutana na mengine, na mengine yale aliyosema mama Teri.
 
Ndani ya CCM tunazo taarifa kwamba hata wenyeviti wa chama, makatibu nao walilipwa rushwa na kusaidia kampeni za wagombea. PCCB na usala wa wilaya hata DCs pia walihusishwa. Wakalamba cha kwao na matokeo yakatoka.
 
Back
Top Bottom