Wajumbe Kamati ya Miss Tanzania waondoka kuelekea Sanya China

Wajumbe Kamati ya Miss Tanzania waondoka kuelekea Sanya China

Mama Mdogo

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2007
Posts
2,967
Reaction score
2,147
Blog ya Issa Michuzi imetoa taarifa kuwa, ujumbe wa watu 5 umeondoka nchini leo kuelekea Sanya China kuhudhuria Tamasha la Miss World 2010. Wajumbe hao ni: (1) Bwana Hashim Lundenga, na Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, (2) Bwana Bosco Majaliwa, Katibu Mkuu wa Kamati, (3) Glory Mwanga - Miss Tanzania 2010 Mshindi wa pili, (4) Anna Daudi, Miss Temeke mshindi wa 2 na ambaye pia alifanikiwa kuingia katika 10 bora ya Fainali za Miss Tanzania 2010, na (5) Mama Mzazi wa Miss Tanzania 2010 Genevieve Emmanuel, Mrs. Mary E. Mpangala.

Ujumbe huu umeondoka nchini leo kuelekea Sanya China katika kuhudhuria mashindano ya urembo ya dunia yaliyopangwa kufanyika Jumamosi Tarehe 30 Oktoba 2010. Ujumbe umeondoka kwenda kushuhudia Fainali hizo za kumtafuta Mrembo wa dunia ambazo zitafanyika Jumamosi hii katika kisiwa cha Hainan huko Sanya China. Msafara huo unatarajia kurejea nchini Tarehe 3 Novemba 2010.

Tumeona na kusikia yaliyotokea kwa timu yetu iliyokwenda India kwenye michezo ya madola, haikurudi na medali yoyote. Uratibu wa viongozi wa msafara ulivyokuwa wa kutia mashaka wakati wakiwa huko, ilifikia hata yule binti mwogeleaji akawasili kwenye bwawa amechelewa!! Walipoulizwa, ilikuwaje, wakajibu, ati unashangaa nini!!! Mbona watu huwa wanachelewa kupanda ndege, sembuse kuogelea!!!.

Imekuwa ni tabia za ujumbe wa Tanzania ukienda kutuwakilisha kwenye michezo, wanaondoka na mizigo haba wakitupa matumaini tele, lakini wanapokuwa wanarudi wanakuwa wamesheheni mizigo tele na visingizio kibao kwa nini wamekosa ushindi. Ka mitindo hii ya kukosa matayarisho pamoja na kukosa stadi na umakini wa kiuongozi, mimi matumaini yangu ni madogo sana kwa Miss Tanzania kurudi na ushindi.


Issa Michuzi_Miss Tanzania P1270016.JPG
 
Waste! yaani wanakera mno! ni uharibifu wa hali ya kuu na ngoja Slaa aje kuwaslaaashhhhh!!
 
Back
Top Bottom