Wajumbe kutoka Zanzibar kupunguziwa posho

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Habari wadau,

Leo nikiwa hapa mjini Dodoma nilipata nafasi ya kuongea na dereva mmoja wa mjumbe wa bunge la katiba ambae pia ni mbunge wa bunge la Jamuhuri kutoka Zanzibar, na akanidokeze kuwa hakuna mpango wa hao waheshimiwa kuongezewa posho na pia kuna mpango wa kupunguza posho kwa wajumbe wa Zanzibar wanaolipwa sh 420,000 kwa siku.

Pia dereva huyo kanidokeza kuwa kwa wale ambao wanaona posho haitoshi wanatakiwa waache.

NB:Hii ni tetesi tu,kwahiyo ichukulie kama ilivyo.
 
Sawa mkuu. Ila hebu nielimishe, hiyo difference ya 120,000 kwa wabunge wa zanzibar wanalipwa na nani? Serikali yao ndo imetop-up au ni toka mfuko huo huo unaowalipa hawa wa tanganyika?
 
wanataka kuwalaghai wadanganyika wasipigekura ya serikali tatu.
 
Sawa mkuu. Ila hebu nielimishe, hiyo difference ya 120,000 kwa wabunge wa zanzibar wanalipwa na nani? Serikali yao ndo imetop-up au ni toka mfuko huo huo unaowalipa hawa wa tanganyika?

Kwa maelezo ya huyo dereva ni kuwa wajumbe kutoka Zanzibar wanalipwa na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar(SMZ).
 
Hawa wadai posho wamewekwa kimkakati zaidi,wanajua wanachokifanya.
 
kihalali hata obama tukiondoa mambo ya usalama hawezi kumaliza laki tatu kwa siku akiwa dodoma,yatajwe majina ya hawa wapuuzi wanaodai nyongeza,najua na wa upinzani wamo kwenye huu mkumbo(sio kitila)
 
kwn jamani kuna makisa kwa smz kuwapa wajumbe wake posho na nyie si muiambie serikali ya tanganyika km ipo iwape?
 
Sawa mkuu. Ila hebu nielimishe, hiyo difference ya 120,000 kwa wabunge wa zanzibar wanalipwa na nani? Serikali yao ndo imetop-up au ni toka mfuko huo huo unaowalipa hawa wa tanganyika?

Kingmairo,
Unahitaji kueleweshwa kwamba wenzetu hao wanatoka nchi ya ugenini? Kule ni nchi nyingine kabisa, wapo ugaibuni hapo Dodoma. Utawalinganishaje na hayo ya Tanganyika? Kama hawatapoozwa na hiyo tofauti, wanaweza kuamua kuukataa muungano na kudai Zanziba huru. Amah!
Wao wanayo Katiba yao, wameletwa kama Matx wanaujuzi mkuu wa kuandika katiba, we vipi? Unaudharau ujuzi?
 

Hah ha ha ha, mkuu sijaudharau u-tx, kwanza mie ni muumini mkubwa wa uskills wa matx. Nlikuwa sina uhakika ni nani hasa anawalipa iyo additional amount. Kama ingekuwa ni mfuko huo huo mmoja unawalipa baadhi 300k na unalipa wengine 420k, ingekuwa sio fair! I mean madai ya hawa wa tanganyika yangekuwa valid.
 
Acheni kuzuga watu, Inaeleweka wazi kuwa mchakato wa katiba ni shinikizo la mataifa na jumuiya za madola. Hiyo pesa pia ni mfuko wa kuisaidia afrika kwa masuala ya maendeleo. Norway na UN wanasaidia katika kuwalipa wabunge wa katiba . Hamna pesa ya tanzania hapo. Ni msaada wa nje.
 

Kingmairo,
Sijui unavyolitizama hili jambo, Uzanzibari unatoka wapi hapa na Utanganyika? Kwa nini Serekali hizo zisielewane namna ya kuwalipa hao wajumbe wanaofanya kazi moja hiyo hiyo? Wanakaa siti moja, M/Kiti wao ni mmoja, sauti wanaisikia ni moja, wakijibu wanajibu swali moja iweje weye ulipwe kitofauti?
Huu ni mpango mahsusi wa kuwaudhi hao Watanganyika waondoke wawaache hao ma tx waifanye kazi njema. Just wait and see.
 
Hapo ndo wajue Tanganyika na Zanzibar ni nchi mbili tofauti zenye malengo tofauti. Laki 3 ndogo? Oh my God! Huyu Ndasa anatumiwa na nani?
 

Sawa. Basi liwekwe wazi kwa Wananchi kuelewa. Haya mambo ya sirisiri ndio hatutaki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…