Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 5,119
- 4,569
Ninadhani mmeshaona kuwa kuna wajumbe wachache katika bunge maalum la katiba IQ zao zina hitilafu na wamekuwa wakimzomea na kumtukana wazi wazi Mwenyekiti wa muda Mzee kificho ambaye hata kwa umri wake tu walipaswa kumheshimu kama baba yao. Wanalifanya Bunge letu maalum la katiba lionekane kama bunge la makangaroo au la vijiweni. Bunge hili halina mamlaka ya kuwashughulikia wajumbe hawa kwani ni wateule (kama ilivyojionyesha kwenye kanuni za bunge hili), na yule aliyewateua sheria haikumpa mamlaka ya kuwashughulikia.
Vyombo vya habari (media) ikiwemo JF, kama mhimili wa nne wa serikali nadhani vinapaswa kwa niaba ya Watanzania wote wenye nia njema kuwaadabisha wajumbe hawa wachache wanaojifanya ma 'much know' kwa kuwasema, kuwazomea n.k. Tuanze kwa kuwataja majina yao hapa. Mmoja niliyembaini anatoka mkoa wa Kigoma, jina lake bado sijalifahamu.