Wajumbe wa Bunge la katiba walitakiwa kupatiwa semina kabla ya kufanya lolote juu ya katiba mpya

Wajumbe wa Bunge la katiba walitakiwa kupatiwa semina kabla ya kufanya lolote juu ya katiba mpya

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Mimi nafikiri tumefanya kosa kubwa kuruhusu hawa wajumbe wa Bunge la katiba kuanza mchakato huu ikiwa ni pamoja na kuandaa kanuni za kuendesha Bunge hilo kabla ya kuwapatia semina maalumu juu ya utungaji na uandikaji wa katiba.

Semina hiyo ingekuwa na mada mbalimbali kama vile nini maana ya katiba,misingi ya katiba,kwanini wao wako pale,nini hasa jukumu na wajibu wao kwenye kuandika na kutunga katiba hiyo,miiko ya katiba, n.k.

Semina hiyo ingeendeshwa na watalaamu wa mambo ya katiba na pengine wangetoa elimu ambayo ingewasaidia katika jukumu lao hilo.Hii mivutano na kutoekewana ndani ya Bunge hili kumechangiwa na kukosekana kwa elimu juu uandikaji na utungaji wa katiba kwa wajumbe hawa

Kwa maneno mengine,wajumbe hawa hawajaandaliwa kisaikolojia kujua wajibu na jukumu lao katika kazi hiyo waliopewa kuifanya.

Labda niulize tu,hivi kama mawaziri waliandaliwa semina kule Ngurudoto Hotel,inakuwaje wajumbe hawa wenye jukumu nyeti kama hili hawakupewa semina ya kuwaweka sawa katika kazi yao?!

Kama swala ni gharama,hivi kuna gharama inayolingana na kupata katiba mbovu?
 
Ni sawa kabisa ,ila kitu kimoja wanaoanzisha vurumai hapo Dodoma katika hilo kutano la BLK ni wale wabunge wazoefu ,wale wageni hawana tofauti na kuku mgeni kama waliofungwa kamba ,mabishano yote kuanzia ya posho hadi kura za wezi ,wabishanao na kuwaonyesha walio wageni kuwa ndio wenyewe.

La muhimu kwa ujumla wao wote wasiwe kama ng'ombe waliofungwa kamba ya puani ,wanaburutwa na wajuaji wa kusema wanaotumia vitisho ,huo utakuwa udhaifu mkubwa ,wananchi wanaamini hapo haogopwi mtu ,sasa wao wakiogopa kutetea na kuhoji mambo yanayojadiliwa na kuamua vile waonavyo wao ndio sawa ,wajumbe hao hawafai hata kuitwa watu.
 
Salary Slip, Mwiba,

..I don't think so.

..idadi kubwa ni wabunge, hao tayari wana uelewa mpana kuhusu katiba.

..walioteuliwa na Raisi pia wengi ni wasomi, na wametokea ktk makundi ambayo yana maslahi na katiba.

..kinachosumbua hapo ni wabunge wa CCM ambao wamejitia uendawazimu kwa kuazimia kuwaburuza wajumbe wengine wa bunge la katiba.
 
Last edited by a moderator:
hivi si nimewasikia wabunge wenyewe wakisema kuwa wamepewa semina? Au we ulitaka kama ile ya ngurdoto?
 
Salary Slip, Mwiba,

..I don't think so.

..idadi kubwa ni wabunge, hao tayari wana uelewa mpana kuhusu katiba.

..walioteuliwa na Raisi pia wengi ni wasomi, na wametokea ktk makundi ambayo yana maslahi na katiba.

..kinachosumbua hapo ni wabunge wa CCM ambao wamejitia uendawazimu kwa kuazimia kuwaburuza wajumbe wengine wa bunge la katiba.

i totally agree with you
 
Hapo ndio palipo na hali ya mjumbe mmoja mmoja kuwa jasiri ,wajumbe hao wa CCM wamepokea amri na kupewa semina na mikakati na kutishwa na vigogo wa ccm ,wanaojiona kama wao ndio wenye hati miliki ya Nchi hii ,ni muhimu kwa wajumbe wa CCM kuepuka vitisho walivyopewa au tuseme ulazima walioambiwa waufanye katika maamuzi ,watambue kuwa waliowambia au kuwalazimisha hawana nia njema na nchi hii.

Na CCM haimthamini mtu ,usisikie uwe mwanachama wao au mbunge wao au kiongozi wao ,katika CCM kama hamuelewi kuna mafia style authority na kuna wakuu flani wengine au wengi wao wameshastaafu ,lakini wana monitor kila kitu na wana amri ,wakiamua kukudozoa wanakuweka kando na kukutupa kwa kishindo. Hiki ndicho kinachoendelea ndani ya CCM ,mliona walifanya semina kibao ,katika vikao hivyo angalia sura za wastaafu flani flani ,na hata wanayoyasema wastaafu hao huwa yanakwenda kwa muelekeo wa vitisho. Ila hapa ipo kazi.
 
Ni sawa kabisa ,ila kitu kimoja wanaoanzisha vurumai hapo Dodoma katika hilo kutano la BLK ni wale wabunge wazoefu ,wale wageni hawana tofauti na kuku mgeni kama waliofungwa kamba ,mabishano yote kuanzia ya posho hadi kura za wezi ,wabishanao na kuwaonyesha walio wageni kuwa ndio wenyewe.

La muhimu kwa ujumla wao wote wasiwe kama ng'ombe waliofungwa kamba ya puani ,wanaburutwa na wajuaji wa kusema wanaotumia vitisho ,huo utakuwa udhaifu mkubwa ,wananchi wanaamini hapo haogopwi mtu ,sasa wao wakiogopa kutetea na kuhoji mambo yanayojadiliwa na kuamua vile waonavyo wao ndio sawa ,wajumbe hao hawafai hata kuitwa watu.

ccm ni balaa. wameshalewa madaraka. suala hapo siyo semina tu. attitude ya waccm siyo nzuri kabisa towards katiba. mpaka wabadilike mtazamo ndo semina ingeweza kusaidia, vinginevyo ni semina bila change of perception, ni sawa na kupaka mafuta kabla ya kuoga na utegemee kuwa msafi. attitude ya waccm ikibadilika na wakawa wazalendo kwa maana ya kuwa objective na wakakubali principle ya give and take, mambo yatatilia na tutaenjoy bunge.
 
Back
Top Bottom