Wajumbe Wa Bunge La Katiba Wawekewe Posho Zao Kwenye Account Zao

Wajumbe Wa Bunge La Katiba Wawekewe Posho Zao Kwenye Account Zao

Kuntakint

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2011
Posts
1,767
Reaction score
1,526
Nimeona picha ya wajumbe wa katiba wakiwa kwenye foleni wakisubiria posho zao. Kwa kweli inatia aibu katika nchi yetu na hasa serikali yetu ni jinsi gani bado tuko nyuma katika ulimwengu wa technolojia. Ni nchi gani umewahi kuwaona viongozi wao, wabunge wanapanga foleni kusubiria pesa? Tanzania tunajua kuimba na kujifanya tunajua kila kitu wakati hatujui.

Ni udhalilishaji mkubwa kwa kuwaweka wajumbe wa katiba yetu kwenye foleni kusubiri posho, wakati wangetakiwa waende wakapumzika na kujiandaa kwa ajili ya kikao cha kesho yake.

Kwanini wasiwekewe pesa zao kwenye akaunti zao. Sidhani kama hawa wajumbe wetu watakuwa hawana akaunti za benki. Kinachotakiwa ni kukusanya mahudhurio ya kila mjumbe ya wiki halafu analipwa pesa yake kwenye akaunti yake ili iwe rahisi kwake kwenda kuchukua kwa wakati wake na hata anaweza kumtuma mke, mume au anayemwamini kwenda kumchukulia kwa muda wake. Na itapendeza kama watalipwa kwa wiki na mahudhurio yao yanakusanywa kwa wiki, hii itawaisaidia sana. Tuachane na zana zile za kutembea na pesa.

Katika ulimwengu wa sasa watu hawatembei na pesa. Wasaidieni wajumbe wetu kwani kazi tuliyowapa ni kubwa.
 
wewe unaonekana hauna mafikilio
kwa nini walipwe wakati ni sehemu yao ya kazi wakati wafanyakazi kama walimu askari wakilipwa mshahara ambao ndio wenyewe wanachukua posho kwao nasema hatuna wawakilishi bungeni tuna wanyonyaji tu
 
Tanzania inasikitisha hata bumu halio hivyp
 
Ww unafikiri kwa kutumia nn? Tatizo lipo wapi wao kupanga foleni,watu wenyewe mmmh hamna kitu
 
Back
Top Bottom