Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Uchaguzi wa Taifa wa CHADEMA, umekuwa ni jambo la heri sana. Ndio uchaguzi uliowafanya watu wengi wayatambue madudu ya baadhi ya viongozi.
Ni uchaguzi uliowaamsha wanachama na viongozi wa ngazi mbalimbali, kutambua kuwa kumbe hata ndani ya CHADEMA kuna takataka nyingi ambazo zipo ndani ya CHADEMA kwaajili ya maslahi. Mambo ya jumla yaliyofichuliwa na uchaguzi huu:
1) Mifumo ya pesa ipo ovyo sana, na kuna kikundi kidogo makao makuu kinajimilikisha pesa ya chama.
2) Kuna watu ndani ya CHADEMA, wanaifanya CHADEMA ni mali yao, na hivyo wanaweza kufanya lolote watakalo, na wengine wote hawatakiwi kusema kitu.
3) Ndani ya chama, miongoni mwa viongozi, wapo wahuni, lakini kwa kuwa wanatumiwa na makao makuu, wanapachikwa kwenye nafasi za uongozi kwenye mikoa na kanda, pamoja na ubuni wao. Ntobi ni mfano mmojawapo..
NB: Uchaguzi wa safari hii ndiyo nafasi pekee ya chama kutoka kwenye mikono ya kikundi kidogo na kukipeleka kwa wanachama wote. Hilo litafanikiwa kwa kuwaondoa wote waliojimilikisha chama na fedha ya chama, kwenye nafasi za uongozi. Na jukumu hilo muhimu na zito lakini lililo muhimu sana, wamepewa wajumbe.
Wajumbe lazima mkumbuke kuwa aliyeyatengeneza matatizo hawezi kuyamaliza. Tunahitaji watu wengine.
MBOWE TUMPUMZISHE.
TUNDU LISU, Heche, na wajumbe wengine kama Rose Mayemba wakabidhiwe uongozi wa chama ili wasimanie mabadiliko