Wajumbe wa Kamati Ya Katiba Mpaya Waache Kulazimisha Agenda Zao Binafsi!!

Wajumbe wa Kamati Ya Katiba Mpaya Waache Kulazimisha Agenda Zao Binafsi!!

Joined
Apr 27, 2006
Posts
26,584
Reaction score
10,400
- Toka siku ya kwanza Kamati hii ilipotoa Rasimu ya kwanza ya Katiba Mpya nilishauri Rais wa Jamhuri kuifutulia mbali hii kamati kwa sababu, imeanza pole pole ku-behave kama Institution badala ya Kamati tu ya kupokea Mapendekezo na kuyaandika chini that is all, ndio kazi yao ya msingi. Lakini nashangaa jinsi wajumbe wa kamati hiyo walivyoanza kujiingiza kwenye kulazimisha wananchi washiriki wa mabaraza yao kukubali hoja zao wajumbe wa Kamati badala ya kusikiliza tu na kuandika mawazo ya Mabaraza huko Mikoani.

- Majuzi nilikuwa Moshi/Kilimanjaro nimeshuhudia Mjumbe mmoja wa Kamati hiyo Butiku akijaribu kwa nguvu nyingi sana kujaribu kuwalazimisha wananchi kukubali Serikali Tatu, mpaka pale Mwananchi mmoja alipomkomalia kwamba Butiku ni lazima amsikilize hoja zake za Serikali Mbili sio kumlazimisha Serikali Tatu, ndipo Butiku aliporudi nyuma, jana again Mjumbe mwingine wa Kamati hiyo Ali Saleh Ali huko Singida yamemkuta kama hayo ya Butiku baada ya kukomaliwa na mwananchi mmoja anayetaka Serikali Mbili huku mjumbe huyo akijaribu kumlazimisha mwananchi huyo kukubali Serikali Tatu.

- Again, hii Kamati muda wake umesha-expire, walitakiwa tu waandike mapendekezo chini na kutuachia Taifa tuhangaike nayo, lakini badala yake wamekuwa mstari wa mbele sana kujaribu kulazimisha wananchi wakubali matakwa yao wajumbe wa tume na sio mawazo yao wananchi, that is bad ni wakati muafaka sasa kamati ikavunjwa na kupewa shukrani kwa kazi njema ya kukusanya maoni kabla hawajatuletea tafrani. Haitakiwi kuwepo na malumbano katika kupokea mawazo ya wananchi sasa yanapokuwepo malumbano baina ya wananchi na wajumbe wa kamati hiyo ni dalili tosha kwamba tutaishia kupata katiba yenye utata, please let them go now kabla hawajtuchanganya zaidi!!,

Le Mutuz Live In Mbeya!!

william
malecela.blogspot.com


Mwenyekiti wa tume ya katiba Ali Saleh Ali mjini Singida akijaribu kutumia nguvu nyingi kumlazimisha mwananchi chini akubali Serikali Tatu.Mjum

- See more at: http://williammalecela.blogspot.com/#sthash.9G4L8Pcs.dpuf
 
Yaonekana umeandika ukiwa MALIWATONI! WaTanganyika sio wajinga ki hivyo kama mnavyo dhani. Yaani mkishaingia humo kwenye lichama lenu mnajazwa ujinga wa kuwaona waTanganyika ni wajinga wakati wote.

Ni nani asiye juwa kwamba MAGAMBA mnataka andiko la Katiba Mpya liwe kama mnavyo taka? Upuuzi wenu ufanyieni kwenye vikao vyenu huko, na sio kwenye maslahi ya waTanganyika.

Umepenya kwenye ujumbe wa Jumuiya ya wazazi basi umesha geuka msemaji wa waTanganyika. Tanganyika ya leo sio ile ya kina Jumanne Malecela.
 
Hao mamluki mliowalisha namna ya kuongea kwa maslahi yenu maccm?? umeona wapi muungano kiini macho kama huu tulionao?? ni aibu kuendeleza longolongo kwa kulinda maslahi yenu..Kuliko huu muungano kubaki kama ulivyo ni heri sana uvunjike.
 
Muungano ambao muundo wa serikali ni wakijinga,haueleweki.Ila naomba sana uangalie kwanza katiba mpya ya Zanzibar kabla haujaja hapa na upuzi wako..Muungano ungekuwa umevunjika rasmi zamaaanii kama CC ya CCM wasingekuwa wanampitisha mgombea wa urais wa Zanzibar wao..Waachieni wananchi wampitishe wenyewe muone ajenda kuu ya kujinadi itakuwa nini...Zaidi ya hayo msalimie mzee Jumannee na muulize kama bado anajiita tingatinga.
 
W.J.Malechela, kamuuliuze mzee, a.k.a Tigatinga, serikari ya Tanganyika iko wapi? kama bado anakumbukumbu ya G55, akikupa jibu uje sasa tujadiliane
 
Huyu jamaa ana uandishi wa ajabu, yaani wa kihunu huni, mlipo hijack utaratibu wa kupata wajumbe mlitegemea nini? Warioba komaa nao tata mpaka kieleweke
 
Hivi unajua hivi unavyo fanaya ni USALITI mkubwa sana......Ni usaliti wa kijinga sana kutetea CHAMA kuliko kutetea nchi.......pamoja na kukaa kote us ....umeshidwa hata kujifunza jinsi wanavyoweka nchi mbele kuliko vyama......TANZANIA TUNA HASARA KUBWA SANA YA BAADHI YA VIJANA...
 
............vipi wale wanaosema kuhusu kuondolewa neno 'tanzania bara' na ili jina Tanganyika lichukue nafasi yake stahili!
 
Huyu jamaa naona hata hela ya bia hana tena kwasababu alichoandika lazima kimetoka kwenye keyboard ya Mnywa gongo na wanzuki
 
LE MUTUZ WITH MY SUPER SISTER SUPER MWANVITA MAKAMBA.
MANVITA.jpg

haya ndio mambo ya le mutuz,siasa haziwezi huyu
 
Sikubaliani na vitendo vya baadhi ya wajumbe wa mabaraza ya katiba kuchangia maoni ya rasimu ya katiba kwa kusoma mapendekezo ya CCM wanapochangia kuboresha rasimu hiyo.
Tume ya Kukusanya maoni ya katiba tayari imeshapokea hayo maoni ya CCm kama maoni ya taasisi, sas hawa wajumbe ambao wamechaguliwa na wanachi ili wakawawakilishe inakuwaje wanaanza kusoma mapendekezo ya CCM badala ya mawazo ya wananchi waliowachagua wakawawakilishe? au walipandikizwa na ccm?
 
LE MUTUZ WITH MY SUPER SISTER SUPER MWANVITA MAKAMBA.
MANVITA.jpg

haya ndio mambo ya le mutuz,siasa haziwezi huyu
Du umenikumbusha mbali sana huyu kaka yangu W. J. Malecela tafadhali achana kabisa na suala la Serikali 2 kwani Zanzibar hawalitaki.
Kuiambia Tume ya Rasimu ya Katiba ya Warioba haifai ni kutudanganya Watanzania Bara, (Watanganyika)
CCM hawajui walisemalo kwani Wazanzibar wote hawautaki Muungano sasa kujidanganya kuwa watapiga kura kuukubali ni hapo kura zitakapokuja kuwaumbua CCM (huwezi ng'ang'ania mke anayekutangaza kuwa hakutaki)
Soma Magazeti ya leo Mwananchi 26/07/2013 na Jamii Forum https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ka-muungano-ufutwe-yaanza-rasmi-zanzibar.html
Zanzibar. Kesi inayotaka Muungano waTanganyika na Zanzibar ufutwe imefunguliwa katika Mahakama Kuu yaZanzibar.
Kesi hiyo iliahirishwa jana MahakamaKuu ya Vuga mjini hapa na Mrajisi wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, George Kazi hadi Agosti 23, mwaka huu.
Mrajisi aliahirisha kesi hiyo iliyofunguliwa na watu 1,950 wa Unguja na Pemba kwa vile Jaji Mkuu waZanzibar, Omar Othman Makungu hakuwapo.
Source: Mwananchi 26/07/2013
 
Last edited by a moderator:
Hivi le mutuz una issue yeyote personal na hawa wazee Warioba na Butiku?nimekufuatilia siku nyingi sana comments zako juu ya hawa wazee!kuna siku ulishawahi sema wanakosoa kwa sababu wana wivu wa kunyimwa vyeo
 
Du umenikumbusha mbali sana huyu kaka yangu W. J. Malecela tafadhali achana kabisa na suala la Serikali 2 kwani Zanzibar hawalitaki.
Kuiambia Tume ya Rasimu ya Katiba ya Warioba haifai ni kutudanganya Watanzania Bara, (Watanganyika)
CCM hawajui walisemalo kwani Wazanzibar wote hawautaki Muungano sasa kujidanganya kuwa watapiga kura kuukubali ni hapo kura zitakapokuja kuwaumbua CCM (huwezi ng'ang'ania mke anayekutangaza kuwa hakutaki)
Soma Magazeti ya leo Mwananchi 26/07/2013 na Jamii Forum https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ka-muungano-ufutwe-yaanza-rasmi-zanzibar.html
Ukiwa mwaccm mara nyingi unakuwa na uchi..zi kidogo, busara hunakosa kabisa. Ni wanaccm wachache sana wana busara na wanatafakari kama ya kuongea au kuandika kitu kwenye mitandao ya kijamii.

Lakini tusiwalaumu sana kale kamsemo kao za "ZIDUMU FIKRA ZA M/KITI WA CCM" kamewaganda kichwani.
 
Huyu jamaa W.J.Malechela aka Le Mtuz ameandika issue hii ya kupinga serikali 3 mara nyingi. Kwa siku ya leo tu tayari amenzisha mada mpya 2 juu ya hili la kukataa serikali 3. Kaa mbali nasi wadanganyika! Safari hii hatudanganyiki kirahisi. Kwenye uzi wa kwanza umepewa shule ya uhakika juu ya uhitaji wa serikali tatu kurekebisha mfumo wa serikali 2 ambao ni wa ajabu. Muungano wa nchi mbili Tanganyika (mfu) na Zanzibar (Hai), kwa nini hazikufa zote au kubakia states chini ya Muungano?
 
Huyu jamaa naona hata hela ya bia hana tena kwasababu alichoandika lazima kimetoka kwenye keyboard ya Mnywa gongo na wanzuki

- Wrong number sijwahi kunywa pombe wala sigara kwenye maisha yangu so take this back!!

Le Mutuz
 
One of the famous hopeless guy!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom